Mwanasosholaiti kutoka Uganda Zarina Hassan ni mama mwenye furaha baada ya bintiye Princess Latifah kutimiza umri wa miaka 8.
Princess Latifa ni binti ya mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platinumz na mwanasosholaiti wa Uganda Zari.
Latifa alizaliwa Agosti 2015 nchini Tanzania, akiwa binti wa watu mashuhuri, Princess Latifah ndiye mtoto anayefuatiliwa zaidi kwenye Instagram katika Afrika nzima.
Mwaka jana wazazi wake walimfanyia sherehe kubwa na ya kifahari nchini Afrika Kusini ambapo kwa sasa wanakaa na familia yake.
Princess Latifah ni binti wa kwanza kwa Zari na mtoto wa kwanza wa Diamond kwani Zari ana watoto wengine kutoka kwa ndoa ya awali.
Ingawa wazazi wake hawapo pamoja tena kwani waliachana, lakini wanashirikiana kwa furaha kuwalea watoto wao.
Mara nyingi wanaonekana wakiwa pamoja hadharani jambo ambalo limekuwa suala kwa mashabiki kwani walidhani bado wako pamoja lakini Zari ameolewa na mwanaume mwingine. .
Kupitia kwebnye ukurasa wake wa Instagram zari alimwandikia Latifah ujumbe wa kipekee huku akishereheka siku hiyo maalum.
"Happy birthday sukari yangu @princess_tiffah 8 looks so pretty on you🎂💕👗@dyna_vence."
Hizi hapa baadhi ya jumbe za mashabiki;
Lavnie: Yani maelezo mafup tu had raha. Ila sisi wabongo tungeandika maelezo marefu tu! Yani tungesimulia stori kipindi unamimba mpka unavyojifungua😂 alafu ndo tungemalizia na heri ya kuzaliwa mwanangu! NWEI HAPPY BIRTHDAY DADA TIFFAH😍
chudy: aka kanapendwa utadhani ye ndio first born vileee😂😂😂
erhakjr: Wawoooooooo....her success"ll be the same like her mumy...team Zari 👑 every where win....happy birth day to the angel Tiffah"🍾🥂🎂🍻
icon: Happiness and joy for the only flower in our garden....happiest birthday to the Dutchess of Tanzania 😍😍😍😍😍❤️❤️❤️❤️❤️❤️
julie: Happiest birthday to the only Princess to Mama Tee and Baba Tee❤️This girl is a shining star✨✨.The world is ready for you,the sweet Tanzanian Dutchess 🔥❤️