Maua Sama na Zuchu waparurana mitandaoni kisa madai ya kununua views YouTube

Zuchu aliibua madai kwamba wasanii wengi wa Bongo wanaishi maisha ya kununua views YouTube ili kuwatisha wenzao kuwa wana ufuatiliaji mkubwa kwenye jukwaa hilo la video.

Muhtasari

• Mwaka jana, msanii Harmonize alisutwa vikali kwa kile kilisemekana kwamab ni kununua views kwa ajili ya wimbo wake aliomshirikisha msanii wake Ibraah kwa jina mdomo.

Maua Sama na Zuchu waparurana.
Maua Sama na Zuchu waparurana.
Image: Instagram

Siku chache baada ya Zuchu kudai kwamba wasanii wa Bongo Fleva wengi wanaishi kwa kununua utazamaji kwenye jukwaa la YouTube, msanii mwenzake wa kike Maua Sama ameonekana kumjibu.

Kupitia Twitter yake, Maua Sama anadai kwamba Zuchu naye ni mmoja wa wanaonunua views lakini sasa amefikia hatua ya kuwaonea wenzake wanaonunua kama yeye wivu.

Zuchu alikuwa amezua kwamba wasanii wengi wa Tanzania wanaishi maisha ya kuigiza kujidanganya kwamba wanaweza fikisha utazamaji Zaidi ya milioni kwenye nyimbo zao YouTube hali ya kuwa wananunua utazamaji huo.

“Nawaza kama msanii unasikia aje kununua viewrs? Ni kama unajijua nafasi yako ila ndio hivyo tena unaficha kimoyo moyo, unajisikia aje yaani,” Zuchu alisema.

Sama kwa jibu lake, alidokeza kwamba Zuchu naye ni mmoja wa wategemezi wakubwa wa robot za kuongeza views ghushi akisema kwamab ameanza kuwaonea wenzake wivu.

“Maisha haya, marobot wamenza kuoneana wivu,” Maua Sama aliandika.

Japo Sama hakumtaja Zuchu, watu wengi kwenye maoni waliona hilo ni jibu la moja kwa moja kwa Zuchu ambaye aliibua wasiwasi wake kuhusu baadhi ya wasanii wa Bongo kununua views, ambapo pia naye hakumtaja mtu.

Tasnia ya muziki wa Bongo katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ikigubikwa na madai kama hayo ya ununuzi wa views mitandaoni, madai ambayo hata hivyo hayajapata kuthibitishwa.

Mwaka jana, msanii Harmonize alisutwa vikali kwa kile kilisemekana kwamab ni kununua views kwa ajili ya wimbo wake aliomshirikisha msanii wake Ibraah kwa jina mdomo.

Wimbo huo ndani ya saa moja baada ya kuachiliwa, ulikimbia na kupata watazamaji Zaidi ya milioni 1.5 ghafl, jambo ambalo lilitajwa na wengi kuwa si la kawaida na wengine wakisema kuwa ni rekodi ambayo haikuwahi kuonekana tena.

Kilichowashangaza wengi ni wimbo huo kuanza kujikokote katika siku za baadae na kumaliza mwezi ukiwa na watazamaji wasiozidi milioni 2.5, licha ya kupata utazamaji milioni 1.5 ndani ya saa moja.

Je, unaamini wasanii wa Bongo wako chini ya shinikizo la kila mmoja kutaka kuonekana kuwa na utazamaji mwingi kwenye YouTube kiasi kwamba wanaishia kununua views?