Elon Musk akataa kuamini video ya mtu anayemfanana, adai ni ukarabati wa A.I - video

Elon Musk alisema kwamba mpaka sasa hajui kama kuna uwezekano wa mtu kumfanana duniani na kusema kijana huyo anayemfanana kwa asilimia kubwa huenda si binadamu wa kweli.

Muhtasari

• Kijana huyo anayemfanana Musk alipakia klipu hiyo ndogo TikTok akionekana kumtania Musk.

• Alikuwa katika muonekano wa bondia na kando yake mtu aliyevaa sanduku kichwani lenye picha ya Mark Zuckerberg.

Elon Musk
Elon Musk
Image: Twitter

Video ya kijana asiye na shati iliyopakiwa na kijana mmoja wa Uchina anayemfanana tajiri wa Tesla Elon Musk, Yilong Ma, imemfanya bilionea huyo kutaka kujua kuhusu uhalali wa mtu huyo.

Musk Jumatatu alijibu video mpya ya kijana huyo iliyotumwa kwenye Twitter, jukwaa ambalo sasa linajulikana kama X.

Katika video hiyo, kijana Ma anaonekana akiwa hana shati na amevaa glovu nyekundu za ndondi. Alionekana pia kuwa na mchezo wa ndondi za dhihaka na mtu aliyevaa sanduku kichwani, na kuchapishwa kwa uso wa Mark Zuckerberg kwenye sanduku.

Video asili ilipakiwa kwenye akaunti ya TikTok ya Ma mnamo Julai 31, jarida la Insider lilibaini.

"X poa sana," Ma alisema baada ya kurusha ngumi kwa Zuckerberg bandia, akimaanisha pambano la ngome lililotarajiwa kati ya mabilionea hao wawili.

Akijibu video hiyo, Elon Musk alisema kwamba mpaka sasa hajui kama kuna uwezekano wa mtu kumfanana katika dunia hii na kusema kwamba kijana huyo anayemfanana kwa asilimia kubwa huenda si binadamu wa kweli bali ni ubunifu tu wa AI – ubunifu ambao unwezesha akili na mawazo ya binadamu kuzalishwa kwa kutumia mashine.

"Bado sijui ikiwa ni kweli au ni mtu anayetokana na AI," Musk aliandika Jumatatu asubuhi.

Hii sio mara ya kwanza kwa Musk kujiuliza kwa sauti ikiwa ‘pacha’ wake wa Kichina anaweza kuwa mtu halisi na sio bandia ya AI.

Video za Ma pia zinaweza kupatikana kwenye akaunti yake ya TikTok, ambapo ana wafuasi zaidi ya milioni moja kwenye jukwaa na kama milioni 22.2 wamependa kwenye video zake.