logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hongera!Eric Omondi na mpenziwe wabarikiwa na mtoto msichana

Alisema kuwa hiyo ni njia tu ya kuchanga pesa ili aweze kuwasaidia watu.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri09 August 2023 - 15:28

Muhtasari


  • Wanandoa hao walitangaza mnamo Julai 22, 2023 kwamba walikuwa wanatarajia mtoto wa kike katika familia yao.

Mchekeshaji Eric Omondi na mpenziwe wamemkaribisha mtoto msichana,alitangaza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Wanandoa hao walitangaza mnamo Julai 22, 2023 kwamba walikuwa wanatarajia mtoto wa kike katika familia yao.

Walitoa tangazo hilo wakati wa tafrija ya kufichua jinsia ya kushtukiza ambayo Omondi aliiandaa pamoja na marafiki zake wa karibu.

Wapenzi hao walitumia maporomoko ya maji kufichua jinsia ya mtoto wao ambaye hakuwa amezaliwa wakati huo.

Video zilizoshirikiwa mtandaoni kutoka kwa karamu hiyo zinaonyesha kuwa wapenzi hao wanatarajia mtoto wa kike.

"Ni Mtoto Msichana,"Eric alisema.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram,alipakia picha ya mwanawe na mpenziwe wakiwa kwenye kitanda cha hospitali na kufichua anaitwa Princess Kyla Omondi๐Ÿ’•๐ŸŒน

Hizi hapa jumbe za mashabiki wakimpongeza mchekeshaji huyo na mpenziwe;

Jessy: ๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘Uncle Mac Jessy is here so Huyu sasa afungwe diapers international ….Nakuja nazo…!!!!

alinur: Congratz new parents in town

eddiebutita: Congratulations Baba Kyla ๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘

nasrayusuff: Aaaaaawwwww๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜congratulations ๐Ÿ˜๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅโค๏ธโค๏ธโค๏ธ

chriskirwa: Congratulations Baba na Mama Kyla ๐Ÿ™๐Ÿ™

 Eric Omondi alifunguka kuhusu jinsi anapanga kutumia mamilioni ya pesa anazolipisha ili kufichua sura ya mtoto wake ambaye bado hajazaliwa.

Wiki iliyopita, mchekeshaji huyo ambaye taaluma yake imegubikwa na utata mwingi alitangaza kuwa anahitaji kulipwa shilingi milioni 50 ili kufichua sura ya bintiye wakati akizaliwa.

“Kuona sura ya mtoto wangu itakuwa ni pesa nyingi sana, ili niifichue sura ya mtoto wangu nipewe shilingi milioni 50. Atakayenipa hizo pesa hata iwe gazeti utaziona hapo. Uso wa mtoto wangu ni mgumu sana kuona,” Eric alisema.

Aliongeza, “Namlipa kiasi hicho kwa sababu ni mtoto wa kipekee, usisahau ni ya Eric Omondi, na kwa kigezo hicho pekee ni milioni 50. Ni mrembo sana, nilimuona jana kwa scan. Tayari wakati anachunguzwa, naweza kumuona akitabasamu tu."

Katika mahojiano ya kipekee na Radio Jambo, Eric aliweka wazi kuwa halipishi kufichua uso wa mwanawe kwa manufaa yake binafsi bali anafanya hivyo kwa ajili ya Wakenya wanaoteseka katika nyakati hizi ngumu za kiuchumi.

Alisema kuwa hiyo ni njia tu ya kuchanga pesa ili aweze kuwasaidia watu.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoยฉ Radio Jambo 2024. All rights reserved