Karibu niache muziki na Mungu baada ya kujaribu kwa miaka 11 bila mafanikio-Msanii Jabidii afunguka

Mwimbaji huyo wa nyimbo za injili alifichua kuwa karibu aachane na muziki wa injili na nusura apoteze imani kwa Mungu

Muhtasari
  • Kulingana naye, alikuwa akisikiliza nyimbo za reggae na hip hop ambazo zimechochea aina ya muziki anaofanya.
MSANII JABIDII
Image: INSTAGRAM

Msanii wa nyimbo za injili Jabidii akiwa kwenye mahojiano ametoa maelezo kuhusu matatizo yake ya utotoni na safari yake katika ulimwengu wa Muziki wa Injili wa Kenya.

Mwimbaji huyo maarufu wa kibao cha 'Makofi' alizaliwa na kukulia Kibera na mapenzi yake kwa muziki yalikuzwa alipokuwa bado katika shule ya msingi.

Kulingana naye, alikuwa akisikiliza nyimbo za reggae na hip hop ambazo zimechochea aina ya muziki anaofanya.

Jabidii alipata umaarufu baada ya kuachia wimbo wake uliokuwa ukivuma sana wa 'shoot satan'.

Mwimbaji huyo wa nyimbo za injili alifichua kuwa karibu aachane na muziki wa injili na nusura apoteze imani kwa Mungu kwa sababu muziki wa injili ulikuwa haumlipii bili.

“Kama msanii wakati huo nilikuwa nahitaji shilingi 30,Turning point yangu imagine…Song yangu ya kwanza kurecord ilikua 2006 alafu 2017, 11 years later sasa ndio God akaleta hio break through. Time naanza kugive up , 2016 nilifanya shoot satan nikaperform Grove 31st kuamkia 2017. 2017 January vitu zikaenda mrama, sa hio matha ameniona hadi nikiperform kwa tv hadi Jimmy Gait amenitafuta tufanye remix, tulifanya though haikumanage kutoka ifika mwezi wa tatu nyumba imefungwa sa hi shoot sa ni biggie inatrend

“2015 ikiisha nilisema God mi nakupatia hii one year hio time nikitafutana na watu wa school mission nipige mission nitafutane na akina nani.

Baada ya kutoa ngoma yake ya kuvutia ya Odi ambayo alishirikiana na mwandishi wa choreographer Timeless Noel alifichua jinsi ambavyo bado hakuweza kuchuma mapato kutokana na wimbo huo ambao ulikuwa maarufu sana mtandaoni kufikia wakati huo.

"Bado nilikuwa mtaani nikifanya kazi duni nikipata pesa kidogo sana ambazo zilitumika kwa chakula, wakati huu bado nilikuwa na malimbikizo ya kodi licha ya wimbo wangu kuwa hewani na kuchezwa kote nchini" alisema.