logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ukijipata unapiganiwa na mke na mamako, jua ushakuwa mdhaifu - Andrew Kibe

"Unawachukua wanawake wote na kuwaangalia moja kwa moja machoni na kuwaambia ‘f**K” nyinyi wote."

image
na Radio Jambo

Makala10 August 2023 - 07:45

Muhtasari


• Kibe alikuwa anasema kuwa kwake yeye, hakuna vile atajipata wanawake wawili wakipigania kukaa na yeye katika sehemu ya mbele ya gari lake.

Andrew Kibe

Andrew Kibe amedai kwamba wanawake ni kama mashetani na mwanamume yeyote ambaye anapiganiwa na wanawake ni mtu dhaifu.

Katika moja ya klipu kwenye podikasti yake kwenye mtandao wa YouTube asubuhi ya Alhamisi, Kibe alisema kwamba kama mwanamume ukijipata mahali ambapo unapiganiwa na wanawake wawili – mama yako na mpenzi au mke wako – basi jua fika kwamba wewe umezingirwa na mashetani na mwisho wako tayari umepata hatima.

“Acha niwaambie jinsi ya kujitoa katika mtego kama huu. Ukijipata katika mazingira ambapo wanawake wawili wanakupigania kila mmoja anataka kuwa karibu na wewe, na mmoja wao ni mama yako na mwingine ni mke wake, hapo hapo unafaa kuelewa kwamba umeshapoteza. Unafaa ukubali kwamba wewe ni mdhaifu kwa sababu umejiingiza katika mtego wa wanawake wawili ambao ni mashetani,” Kibe alisema.

“Kama mimi ningekuwa wewe nawapiga teke wote na kuendesha gari langu niondoke hapo. Unawachukua wanawake wote na kuwaangalia moja kwa moja machoni na kuwaambia ‘f**K” nyinyi wote pata kila mmoja njia yake ya kwenda kama hamwezi kuwa watulivu karibu na mimi,” aliongeza.

Kibe alikuwa anasema kuwa kwake yeye, hakuna vile atajipata wanawake wawili wakipigania kukaa na yeye katika sehemu ya mbele ya gari lake.

Kibe ameendeleza injili yake kwa watoto wa kiume dhidi ya kutokubali kuchukuliwa maamuzi muhimu na wanawake wao kwa jina la mapenzi.

Mkuza maudhui huyo ambaye yuko nchini Marekani amejizolea jina kutokana na maudhui yake ambayo muda mwingi huchukuliwa kama ya kupotosha wanaume na kuwadhihaki wanawake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved