Jamaa uko miaka 40 na unataka kufurahia ndoa? tafuta mrembo wa miaka 20 - Kibe ashauri

"Wewe ndio unampa mafunzo jinsi ya kuishi. Hawezi shika simu yako, hawezi kuuliza uko wapi umechelewa kufika kwa nyumba, akiwa na wewe ana furaha Zaidi ya kila kitu kwa sababu ni bahati kwake."

Muhtasari

• “Wanawake wenye umri wa miaka 30 wengi wamechoka, wamebeat. Na sio tu kuchoka kiakili, wamechoka"

• "Pengine alianza kutendwa kimapenzi akiwa na umri wa miaka 18 kwendelea mpaka wewe unamkuta akiwa na 30…” Kibe alisema.

Andrew Kibe
Andrew Kibe
Image: Screengrab

Mwanablogu mwenye utata Andrew Kibe ametoa ushauri kwa wanaume waliogonga miaka 40 kwenda mbele na ambao wanatamani kupata ndoa na kutulia.

Kupitia podikasti yake kwenye YouTube, Kibe alishauri kwamba wanaume hao ambao katika umri huo wengi wanatafuta furaha, utulivu na Amani ya akili kuliko kitu kingine chochote katika ndoa wanafaa kufanya maamuzi ya maana kwa kuoa wasichana ambao ndio mwanzo wametia guu kwenye umri wa miaka 20.

Kibe alisema kwamba mwanaume wa miaka 40 kwenda mbele ukitafuta mrembo wa miaka ya mapema 20 huyo atakuheshimu na atakuwa anakuona kama mtu mzima uliyejitolea kumpa maisha ya ndoto yake, hivyo zile dharau nyepesi si rahisi kuziona kutoka kwake.

“Kama wewe ni mwanamume umejijenga kimaisha, uko katika miaka yako ya 40 kwenda mbele, enda uchukue mrembo ako miaka 20, wewe ndio unamfundisha. Wewe ndio unampa mafunzo jinsi ya kuishi. Hawezi shika simu yako, hawezi kuuliza uko wapi umechelewa kufika kwa nyumba, akiwa na wewe ana furaha Zaidi ya kila kitu kwa sababu ni bahati kwake kuwa karibu na wewe. Ukimchukua umpeleke mtoko, anakusifia hadi uchoke, anakurukia. Wachana na hawa wengine wamegonga miaka wanakuuliza kama utakula,” Kibe alishauri.

Kibe alisema kwamba warembo ambao wamegonga miaka Zaidi ya 30 wengi wao wamechoka sit u kiakili bali pia kimwili kwani wengine kulingana naye katika umri huo wengi wamepitia maisha ya kila rangi haswa katika mzunguko wa mapenzi wametendwa sana.

“Wanawake wenye umri wa miaka 30 wengi wamechoka, wamebeat. Na sio tu kuchoka kiakili, wamechoka na… unajua ni mara ngapi amevunjwa moyo kimapenzi? Huyu dem utampata ako na PTSD nyingine huwezi kumudu. Pengine alianza kutendwa kimapenzi akiwa na umri wa miaka 18 kwendelea mpaka wewe unamkuta akiwa na 30…” Kibe alisema.