logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bahati, Diana Marua wamsherehekea mwanao Majesty akifikisha umri wa miaka 4

“Siamini kama wewe si mtoto tena, ukikua mbele ya macho yetu unakuwa Mwanaume taratibu... "

image
na Radio Jambo

Yanayojiri14 August 2023 - 10:47

Muhtasari


• Kwa upande wake, Diana Marua alimsherehekea mwanawe akisema kuwa alimfanya kujihisi mama aliyekamilika.

• “Siwezi kueleza furaha inayoletwa na kuwa Mama yako. Ni uzoefu ambao sitawahi kufanya biashara kwa chochote" - Diana.

Bahati, Diana Marua na mwanao

Familia ya maceleb ya Bahati na mkewe Diana Marua wamemsherehekea mwanao Majesty kwa ujumbe maridhawa leo hii ambapo ametimiza umri wa miaka minne.

Wawili hao walipakia rundo la picha kweney Instagram na kumuandikia mwanao ujumbe maridadi wa kukumbukwa.

“Siku hii Miaka 4 iliyopita nilikuwa Mtu mwenye furaha zaidi Duniani; Nikawa Baba kwa Mtoto wa Kiume anayeruka na tukakupa jina la MAJESTY!” Bahati aliandika.

“Siamini kama wewe si mtoto tena, ukikua mbele ya macho yetu unakuwa Mwanaume taratibu... A Handsome Genius just Like Daddy 😉” aliongeza.

Akirudia ahadi ile ile ambayo alitoa kwa binti yake na mzazi mwenzake Yvette Obura, Bahati pia alimuahidi mvulana wake kuwa atakuwa naye kila mahali na kumuunga mkono katika chochote kila ambacho atachagua kukifanya katika maisha yake mbeleni.

“Ahadi yangu kwako unapofikisha miaka 4 ni kwamba nitakuwa hapa kila wakati kuunga mkono ndoto zako. Nitajitahidi kila wakati kutoa Maisha ambayo sikuwahi kuwa nayo na zaidi ya yote nitakupa Zawadi bora kabisa ambayo Baba anaweza kumpa Mwanae... NITAKUAMINI DAIMA MJ,” Bahati aliandika.

Kwa upande wake, Diana Marua alimsherehekea mwanawe akisema kuwa alimfanya kujihisi mama aliyekamilika.

“Siwezi kueleza furaha inayoletwa na kuwa Mama yako. Ni uzoefu ambao sitawahi kufanya biashara kwa chochote. Nina na bado nazungumza na Mungu juu yako na maombi yangu ni kwamba akupe afya njema siku zote za maisha yako, Akuite Neema na Neema na ayazunguke maisha yako kwa Furaha, Upendo na Utele,” aliseMA Diana.

Diana ni mama wa watoto watatu mpaka sasa ,akiwa na binti wawili na kijana mmoja.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved