Mchekeshaji DJ Shiti amekanusha madai ya hivi majuzi kwamba amefukuzwa nyumbani na mwenye nyumba wake.
Muigizaji huyo wa zamani wa Real House Helps of Kawangware alisema alijiruhusu kufikia hatua hiyo kwa sababu anajua alichokuja kufanya Nairobi.
“Kwa kweli ikifikia hatua na mwenye nyumba ana…tunajua nini ilituleta hapa Nairobi. Sisi tulikuja Nairobi kutafuta na that’s the last thing inaweza kufikia DJ Shiti ishatoka kuwa mtu mmoja ni taasisi sasa yenye kuleta watu wengi sana juu yake haiwezi kufikia hapo. Siwezi kubali ifikie hapo,” alisema kwenye mahojiano na Plug TV.
Kulingana naye, amejipanga na mpiganaji ambaye amejifunza mbinu bora zaidi katika tasnia ya vichekesho.
"Mimi nimejipanga. Mimi ni mapambananji. Mimi ni mtu wa mpango. Mi nimelearn kutoka kwa walio bora zaidi, nimelearn kutoka kwa Daniel Ndambuki, Phelix Oduor ambaye ni mbunge sahizi. Nimejifunza kutoka kwa nahodha Otoyo, MC Jessy, nimejifunza kutoka kwa walio bora zaidi kwa hivyo kufeli ni msamiati, hicho ndicho kitu cha mwisho kinaweza kutokea kwa maisha yangu,” DJ Shiti alisema.
Walakini, hii sio mara ya kwanza kwa ripoti kama hizo kuibuka.
Miaka michache nyuma, Ringtone alidai kuwa DJ Shiti hana makazi katika chapisho ambalo pia aliwadharau watu wengine mashuhuri.
Baada ya kukanusha madai hayo wanamitandao walikuwa na haya ya kusema, huku wengi wakiwakejeli watu mashuhuri;
jones: Don't trust maceleb hapa nje 🤣🤣 anything for clout
mwas: Nyie maceleb mkiwa na pesa mnakiburi sana mkisota mnatukujia tuwachangie daaah
wairimu: Mbona most celebs don’t invest on buying houses or apartments?
msafi: Bro na uko kwa crown wachaizo kuja nikupe mchongo 👌
bear: harufu ya ufukara kila mahali😂😂 literally