Khaligraph afichua siri ya Kiingereza chake kuwa kizuri licha ya kutosoma sekondari

Alipenda sana kuwafuatilia marapa nguli wa Marekani Eminen na 50 Cent ambao amejifunza mengi kutoka kwao jinsi ya sio tu jinsi ya kurap kimuziki lakini pia jinsi ya kutamka maneno ya Kiingereza

Muhtasari

• Khaligraph alianza muziki wake wa kurap akiwa shule ya msingi akisema kwamba asili ya familia yao ina watu wengi wenye wana mapenzi katika muziki.

 
• Jones alikumbuka kwamba zawadi yake ya kwanza kushinda ni katika shindano la kurap akiwa shule ya msingi.

Khaligraph Jones.
Khaligraph Jones.
Image: Screengrab

Msanii namba moja wa muziki wa Hip Hop na rap nchini Kenya Khaligraph Jones amefichua siri ya ubora ya Kiingereza anachokizungumza licha ya kukiri kwamba hakuweza kuhudhuria masomo ya shule ya upili kw asana.

Katika mahojiano na mwanablogu Oga Obinna, Khaligraph alisema kwamba yeye aliishia shule ya upili baada ya karo kukosekana na kuendeleza masomo yake, lakini pia akasema kuwa ubora wake wa Kiingereza umetokana na kufanya mazoezi.

Papa Jones, kama anavyojiita kwa jina la kimajazi alisema kwamba kutoka zamani akiwa mdogo, alipenda sana kuwafuatilia marapa nguli wa Marekani Eminen na 50 Cent ambao amejifunza mengi kutoka kwao jinsi ya sio tu jinsi ya kurap kimuziki lakini pia jinsi ya kutamka maneno ya Kiingereza kwa kiimbo cha Kimarekani.

Khaligraph pia alisema amekuwa akijikita katika kusoma baadhi ya vitabu ili kujiboresha katika matamshi ya Kiingereza.

“Mmabo yangu ya kimasomo yaliishia tu shule ya upili baada ya kuvuka kutoka shule moja hadi shule nyingine. Kiingereza changu ni cha Kayole tu, Kiingereza ni lugha yoyote ambayo mtu yeyote anaweza kuzungumza. Ni hali tu ya kujitolea kujiboresha katika matamshi ya maneno na vitu kama hivyo. Halafu pia vishawishi vyangu, vitu ambavyo nimekuwa nikisikiliza tangu nikiwa mdogo, nimesoma vitabu…,” Khaligraph alisema.

Hata hivyo, Khaligraph alikiri kwamba hajaipata rahisi kwani akikua wengi walikuwa wanamsuta kwamba Kiingereza chake ni feki, akisema kuwa hata sasa hivi bado kuna watu wanaomsuta kwa njia hiyo.

“Nikujifunza tu lugha, uhalisia kwamba sikuweza kufanya vizuri na kwenda kujiendeleza masomo haimaanishi mimi nilikuwa mjinga. Mimi kutoka siku ya kwanza shuleni nimekuwa mtu wa A lakini nililazimika kukatiza masomo kwa sababu hakukuwa na pesa ya kulipa karo,” alisema.

Khaligraph alisema kuwa sasa hivi watu wengi wanamuona kwamba aliishi maisha ya kifahari tangu mdogo lakini akasema kwamba hawakuwa nacho saana kama ambavyo wengi wanamuona.

Khaligraph alianza muziki wake wa kurap akiwa shule ya msingi akisema kwamba asili ya familia yao ina watu wengi wenye wana mapenzi katika muziki.

Jones alikumbuka kwamba zawadi yake ya kwanza kushinda ni katika shindano la kurap akiwa shule ya msingi.