logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Harmonize amfufua Kanumba kumsaidia kumchana vikali Kajala kisa zawadi ya gari

Harmonize alisema amemuachia Kajala zawadi ya gari aina ya Range aliyomnunulia.

image
na Davis Ojiambo

Burudani18 August 2023 - 07:07

Muhtasari


  • • Kanumba japo ndiye alimpa kuhusa ya kumuomba kitu chochote alionekana kushikwa na kigugumizi kwa ombi hilo huku akiishiwa na maneno.
  • •Kanumba walikuwa wanaigiza na Kajala kama mke na mume kwenye filamu zake nyingi.
Harmonize atumia Klipu ya Kanumba kushambulia Kajala

Siku chache zilizopita, Harmonize baada ya kuachia wimbo wake wa Dear Ex alimchana vibaya sana aliyekuwa mpenzi wake Kajala Masanja lakini pia na binti yake.

Baada ya kutoa wimbo huo, kilichofuata ni mashambulizi kutoka pande zote mbili, kisa zawadi na fadhila walizofanyiana, Harmonize akidai kwamba Kajala na binti yake ni matapeli wakubwa walionuiwa kumfilisisha na kumsafirisha kutoka mjini kwenda kijijini.

Msanii huyo alikwenda mbele akisema kwamba aliwasitiri pakubwa kwa kumpa zawadi ya gari aina ya Range Rover akisema kwamba hata haoni vibaya kwan ialifanya tu kwa kuwasaidia na wala hakulihitaji kurudishiwa gari hilo.

Baadae alikuja kusema kwamba ameacha kunywa pombe, kwani awali alidai kunywa pombe kulimpa nafasi nzuri ya kuropokwa maneno dhidi ya Kajala na bintiye.

Lakini licha ya joto la ugomvi wao kuonekana kupunguza kasi, Harmonize ameendelea kumpiga Kajala vijembe vya chini kwa chini akiviambatansiha na figisu figisu kuhusu zawadi ya gari alilompa Kajala.

Safari hii Harmonize ametumia klipu ya zamani ya mwigizaji Kanumba akiwa anaigiza na Kajala ambapo kwenye scene hiyo Kajala alikuwa anamuomba zawadi ya gari.

Katika klipu hiyo, Kajala alimuomba Kanumba – ambaye alikuwa anaigiza kama mume wake – kumnunulia zawadi ya gari la peke yake akisema kwamba alikuwa amechoka kumuazima la kwake kwenda katika mitikasi yake.

Kanumba japo ndiye alimpa kuhusa ya kumuomba kitu chochote alionekana kushikwa na kigugumizi kwa ombi hilo huku akiishiwa na maneno.

Sasa Harmonize kwa kuleta muktadha alionesha kwamba Kajala kutoka kitambo alikuwa akitamani zawadi ya gari kwenye maigizo na yeye ndiye alikuwa mtu wa kwanza kumtimizia ndoto yake katika uhalisia – kwa kumpa zawadi ya gari aina ya Range.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved