Mrembo Georgina Njenga kwa mara ya kwanza amefunguka kwa undani kilichosababisha yeye kumuacha mpenzi wake wa muda Baha Machachari maarufu kama Tyler Mbaya.
Katika mahojiano na Eve Mungai, Georgina amesema kwamba kilichosababisha yeye kuachana na baba mtoto wake ni wote walifikia hatua ya kuchoka na mwingine tu kutokana na mambo mengi ambayo yalikuwa yamerundikana.
“Hakukuwa na sababu ya maana, ni ile tu uhusiano wetu haukuwa unaenda vyema. Si eti naweza kuja nisema kwamba alifanya hivi ama mimi nilifanya hivi, ni masuala mengi tu yaliyorundikana, inafika tu mahali mnagundua kwamba hili haliendi mahali, mwanzo hakuna mwingine aliamua kwamba nimeuacha, ni uamuzi wa pande zote mbili kwamba hatuwezi endelea tena,” Georgina alisema.
Alisema kwamba waliketi chini na Baha na kuelewana kwamba penzi lao tena haliwezi likapiga hatua nyingine Zaidi kwani tayari kitumbua kilikuwa kimeingia mchanga.
“Ni yale tu maongezi tukajadiliana tunaona enyewe hakuna lingine, ni kuachana tu! Sisi wote tulikuwa tunahisi kwamba tungejaribu kutafuta suluhu hadi kwa wazazi lakini haikuweza kabisa,” alisema.
Mrembo huyo alisema kwamba ni kweli hakusonga mbele na maisha bali jamaa aliyemuonesha ni rafiki yake tu, akisema kwamba bado hajapata mtu.
Georgina alisema kwamba kwake yeye, mtoto si kigezo cha mtu kuendelea kuwa katika uhusiano ambao tayari mapenzi yake yamekauka.
“Mimi binafsi nahisi mtoto hafai kuwa sababu ya mtu kuganda kweney uhusiano kama mambo yamekataa kwenda katika njia nzuri, watu wengi wanafanya hivyo. Muda wote mnaweza sidiana kulea mtoto na Tyler anapenda mtoto wake, ako katika maisha ya mtoto wetu katika asilimia mia, na tuliwahi sema kwenye video kwamba hata kama tungeachana baba mtoto wangu lazima tu angekuwa kwenye maisha ya mwanetu. Katika uhusiano, usikae kwa sababu ya mtoto bali kwa sababu uko na furaha,” Georgina alitoa ushauri wenye utata,