logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mtaheshimu watoto lini?-KRG The Don asikitika baada ya wanawe Bahati kukejeliwa mitandaoni

"Upumbavu huu unatakiwa ukome sasa!!" Wanyama alisema.

image
na Radio Jambo

Burudani21 August 2023 - 16:07

Muhtasari


  • KRG ambaye ni rafiki wa karibu wa familia ya Bahati kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amelaani kitendo cha watoto wa Bahati kukejeliwa akisema kuwa watoto wanahitaji kulindwa.
  • Msanii huyo pia alisema kwamba watoto wanapswa kupewa heshima kwani ndio viongozi wa kesho.
KRG atoa tamko lake kuhusu maandamano.

Kufuatia kejeli kali zilizoikumba familia ya Bahati, ikihusisha picha zinazosambaa mtandaoni moja ambayo mke wa Bahati alikuwa amevalia kwa namna ambayo wengine waliiona isiyofaa kwenye picha na mwanawe na katika nyingine, watoto wote wa Diana walikuwa wakifananishwa na wanaume wengine wanaofanana na kudai kuwa ni baba yao.

KRG ambaye ni rafiki wa karibu wa familia ya Bahati kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amelaani kitendo cha watoto wa Bahati kukejeliwa akisema kuwa watoto wanahitaji kulindwa.

Msanii huyo pia alisema kwamba watoto wanapswa kupewa heshima kwani ndio viongozi wa kesho.

"Mtajifunza lini kuwaheshimu watoto katika Nchi hii?mnaweza kunikejeli vile mnataka au watu wengine ambao wamekomaa lakini watoto wa mtu is a no go zone,wekeni heshima kidogo,watoto ndio maisha ya kesho kwa hivyo tunapaswa kuwalinda kwa chochote kile dhidi ya vitu kama hivyo,"KRG Amesema.

Huku hayo yakijiri mwanakandanda,Wanyama alivunja kimya baada ya kufananishwa na mwanawe Bahati Morgan.

Kwa muda mrefu, Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakimfananisha mchezaji huyo wa CF Montreal na mtoto huyo wa Bahati wa kulea na kuibua maswali mengi bila majibu.

Siku ya Jumapili, kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 32 hatimaye alivunja kimya chake kuhusu suala hilo alilotaja kama 'upumbavu' na kuwataka Wakenya kukoma kumhusisha na mvulana huyo wa miaka 13.

"Upumbavu huu unatakiwa ukome sasa!!" Wanyama alisema.

Mwanasoka huyo alieleza hisia zake kwenye mtandao wa Twitter baada ya mwanamtandao kuweka picha yake karibu na Morgan kwenye picha ya familia ya Bahati.

Kwa upande mwingine, mkewe Bahati, Diana Marua alimsherehekea mtoto huyo wake wa kulea na kumhakikishia kwamba anampenda sana.

Mama huyo wa watoto watatu alishiriki picha yake na Morgan na akachukua fursa hiyo kujivunia ukuaji wake.

"Yule aliyeniita MUMMY kwanza. Mtoto wangu @morgan_bahati ni mzima. Mummy and son goal. Nakupenda Morgan," Diana Marua aliandika.

Mapema mwaka huu, Diana alisema ameona maendeleo na mabadiliko mengi kwa Morgan na kumtakia mwongozo wa Mungu maishani.

"Nimekuona ukibadilika na kuwa Muungwana uliye leo na kitu ninachoweza kusema ni kwamba Mungu aendelee kukulinda na aniongoze mimi na Baba yako siku zote tuweze kukulea ili uwe toleo bora kwako," alisema Januari.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved