Malkia ya Bongo Fleva Nandy kwa mara ya kwanza ameonesha sura halisi ya mwanawe na Billnass akifikisha umri wa mwaka mmoja.
Nandy ameweka wazi kwamba mwanawe ni binti ya anaitwa Kenaya na amemsherehekea kwa ujumbe mrefu wenye makopakopa akisema kwamba kumzaa lilikuwa jambo la furaha ribo kwenye maisha yake.
“Mwanangu KENAYA .. siku kama ya leo ndo siku nilipata nguvu ya kukushika mikononi mwangu kwa mara ya kwanza furaha niliyo kuwa nayo haielezeki na wala sijawahi kuipata maishani mwangu tangu nazaliwa,” Nandy aliandika.
Msanii huyo alisema kwamba kila hatua ambayo amepiga na mwanawe si kwa uwezo wake bali ni kutokana na juhudi ambazo Mungu amekuwa akiweka juu ya uwepo wake.
“Umekuwa furaha na faraja kubwa sana kwenye familia, umekuwa mtoto mwenye baraka mikononi mwetu. Baba yako amenifundisha mapenzi lakini wewe umenifundisha jinsi ya kuyaishi mapenzi ya dhati.. nakupenda sana na nakuombea ukue kwenye mikono ya MUNGU!”
Nandy aliomba Mungu kumfanya mwanawe kuwa wa mfano wa kuigwa katika maisha ya baadae akisema kuwa yeye na babake mtoto – Billnass – wanazidisha dua kuishi miaka mingi ili kuweza kuona mafanikio ya uzao wa kwanza wa tumbo lake.
Mwaka jana kuelekea kuzaliwa kwa Kenaya, Nandy aliweka wazi kwamba hakuwa na nia yoyote ya kumfungulia mwanawe akaunti za mitandao ya kijamii wala kumuonesha sura yake mitandaoni.
Msanii huyo amekuwa akihifadhi sura ya mwanwe mbali na kamera za mapaparazi kwa muda wote huu, ikiwa ni pamoja na kuficha jinsia na jina.
Miezi michache iliyopita hata hivyo alionekana na mtoto mwenye rangi ya ngozi nyeusi ambayo iliibua hisia mseto kutoka kwa baadhi ya watumizi wa mitandao ya kijamii wengine wakizua kwamba si mtoto wake na wengine wakimsuta kwamba alikuwa amejichubua ngozi yake.
Lakini katika picha ya mtoto wake halisi ambaye amempakia, kwa asilia kubwa ana ufanano naye na Billnass.