logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nyanya,60, aliyetoka kimapenzi na mvulana,27, alia akikiri ilikuwa kiki, aomba msaada!

Kwa kilio, alisema kwamba kijana yule hata senti moja hajamlipa.

image
na Radio Jambo

Habari21 August 2023 - 12:37

Muhtasari


• “Naomba mnisaidie angalau nitoe filamu zangu nifute machozi maana mimi ni msanii nimecheza filamu,” alimaliza.

• Alisema kwamba yeye ni muigizaji wa muda mrefu na maneno pamoja na vitendo vyote alivyovionesha kwenye sakata zima lililowakunisha wengi vichwa alikuwa ameandikiwa tu.

Kijana wa miaka 27 akimbusu bibi wa miaka 60.

Ajuza wa miaka 60 aliyegonga vichwa vya habari wiki kadhaa nyuma kutokana na penzi lake na kijana wa miaka 27 amerejea tena, safari hii akifunguka ukweli wote kuhusu mahusiano hayo yaliyozua ukakasi mwingi.

Mkongwe huyo amekiri kwamba hawakuwahi kuwa kwenye uhusiano wa mapenzi na kijana yule bali ilikuwa ni kiki tu ambayo kijana alimfuata akimuomba kuidandia ili kupata umarufu.

Ajuza huyo amewaomba watu msamaha kwa kuwaaminisha kwamba alikuwepo kwenye uhusiano wa kimapenzi na kijana huyo – jambo ambalo amelitaja kuwa sio kweli.

"Naomba radhi kwa hiki kitu kilichokuwa kinaendelea naomba msamaha kwa niliowakwaza mimi ni binadamu kama wao naomba wanisamehe sana, nataka niongee ukweli kwamba hiki kitu kilichokuwa kinaendelea mtandaoni kusema kwamba yule kijana ni mpenzi wangu, siyo kweli," alisema.

"Yule ni kama mjukuu wangu, ni kama mwanangu, ila yeye alinifata mimi akaniambia mama wewe si msanii? nikamwambia ndio mimi ni msanii, akaniambia nina wimbo wangu niliurekondi muda mrefu nataka niutoe, nataka tuigize wewe uwe mpenzi wangu nikuoe, akaniambia atanilipa pesa nikikubali kufanya hivyo, basi kwakuwa mimi ni msanii nilikubali nikaamua kufanya kama alivyotaka,” alinukuliwa na media za nchini Tanzania.

Alisema kwamba yeye ni muigizaji wa muda mrefu na maneno pamoja na vitendo vyote alivyovionesha kwenye sakata zima lililowakunisha wengi vichwa alikuwa ameandikiwa tu.

Kwa kilio, alisema kwamba kijana yule hata senti moja hajamlipa.

“Yale maneno yote niliyokuwa naongea nilikuwa naandikiwa, nimeamua kusema ukweli kwasababu nimeona nazidi kutrend hadi nchi za nje lakini hakuna ninachokipata, hajanilipa hata senti tano,” alisema.

Aliomba msamaha pia kwa familia yake ikiwemo wanawe kwa kuwadhalilisha na pia kuomba msaada kwa yeyote kumwezesha kihela kutoa filamu zake, akisema yeye ni muigizaji wa muda mrefu.

"Ni uongo, mimi mume wangu hajafa yupo hai ila tulishatengana, nina watoto wanne tu ambao nimewaumiza sana kwa hiki nilichokifanya mpaka wanalia, nimedhalilika mimi, naomba mnisaidie sina kitu, yale magari na nyumba za kisasa tulikuwa tunaenda kupiga picha tu hakuna mwenye gari kati yangu mimi na yeye."

“Naomba mnisaidie angalau nitoe filamu zangu nifute machozi maana mimi ni msanii nimecheza filamu,” alimaliza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved