Wasanii mibabe wa muziki wa bara la Afrika kutoka Magharibi hadi Mashariki, Burna Boy, Davido na Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza wamekutana wote watatu kwenye tamasha moja la Afronations huko Detrooit nchini Marekani.
Tamasha hilo lilifanyika wikendi iliyopita liliwakutanisha mastaa miongoni mwao Diamond Platnumz, Davido, Burna Boy, PSquare, Mr Flavour pamoja na wengine wengi.
Baada ya tamasha kukamilika, timu ya mpira wa vikapu nchini humo kutoka kwa jimbo la Michigan likakopatikana eneo la Detroit maarufu kama Detroit Pistons iliwatambua mastaa hao kwa kuwapa jezi zao wasanii wanne – Davido, Burna Boy, Diamond Platnumz. Lennox na Letto.
Jezi hizo za NBA zote zilikuwa zimepigwa chapa kwa majina ya wasanii hao. Jezi ya Diamond ilikuwa imechapishwa kwa jina lake la kimajazi ‘Simba’
Ukurasa wa Instagram wa timu hiyo ya NBA ulipakia picha za wasanii hao waliopewa jezi na kusema kwamba waliona ni vyema kuwatambua kwa kuwapa zawadi za kulikumbuka tamasha hilo.
“Afronations ilikuja katika jiji letu na tulihakikisha kwamba lazima tungekuwa na mashiko ya kukumbukwa kwa baadhi ya wageni,” waliandika.
Wasanii hao walikwenda kutumbuiza wakati ambapo mwenzao Wizkid aliyetarajiwa kuhudhuria tamasha hilo kupatwa na msiba wa kifo cha mamake.
Burna Boy na Davido wakiwa katika tamasha hilo, walituma risala zao za rambirambi kwa Wizkid wakimfariji kwamba wanamuombea sana kipindi ambacho anapitia wakati weney ukungu mkubwa Zaidi.
Mamake Wizkid alifariki Ijumaa usiku na ilisemekama kwamba lilikuwa ni pigo kubwa kwa Wizkid ambaye siku zote alikuwa anamtaja mamake kama nguzo muhimu sit u katika maisha ya ukuaji wake bali pia katika safari yake ya muziki.