Kibe asema hana fikira za kuoa na kushauri wanaume kuikwepa ndoa, "Ni makalio ya shetani!"

“Wasichana wengi wanapenda maswali mengi ya kijinga, sitaki. Halafu pia kuna ule muda hutaki kushiriki mapenzi na yeye ndio anataka, ni lazima tu ufanye, mimi siwezani na hayo maisha,” alisema.

Muhtasari

• “Nawambia sasa hivi wanaume angalia mbele uone nyota yako, andika chini hiyo ndoto ya maisha yako ya kesho na uone kama kuna mwanamke hapo, huwezi ona,” alimaliza.

Andrew Kibe
Andrew Kibe
Image: Screengrab

Mwanablogu wa YouTube Andrew Kibe amerejelea msimamo wake kwamba katika maisha yake, hawezi kuingia katika ndoa tena.

Kibe ambaye yuko nchini Marekani katika moja ya podikasti zake amesema kwamba hawezi kumtafuta mwanamke wa kumuoa na kusema kwamba vile alivyo kwa sasa anafurahia maisha na haoni kitu ambacho anakikosa na ambacho mwanamke atakuja kukiongeza kwenye ladha ya maisha.

“Mimi sitaki bibi tena, siwezi kuwa na mwanamke tena, sioni haja ya kupata mke, tufanye nini na yeye? Ni nini ambacho ninakifanya katika maisha yangu sasa hivi ambacho kinahitaji msaada wa mwanamke?” Kibe aliuliza akisisitiza msimamo wake.

Kibe kwa msimamo wake alisema kwamba mwanamke katika maisha ya mwanamume ni kama kivuruge anayekuja na kumtoa mume kwenye ramani ya njia kuu ya kumchukua vichochoroni.

“Unajua wakati mwanamke anakuja kwenye maisha ya mwanamume, kila kitu kinapotea. Mimi nitakuwa sina uwezi wa kuendelea kuendesha hii podikasti yangu,” Kibe alisema.

Mwanablogu huyo anayesuta vikali mahusiano aidha alikuwa na sababu za msimamo wake huo unaoonekana wa kushangaza katika jamii.

“Wasichana wengi wanapenda tafrija, mimi siwezani, halafu kuna maswali mengi ya kijinga, sitaki. Halafu pia kuna ule muda hutaki kushiriki mapenzi na yeye ndio anataka, ni lazima tu ufanye, mimi siwezani na hayo maisha,” alisema.

Kibe aliwashauri wanaume haswa vijana kutokimbilia mahusiano akisema kwamba wanawake huwapoteza wanaume na badala yake wanafaa kutumia muda wa ujana wao kutafuta pesa – “pesa ndio dawa ya Amani na utulivu wa akili.”

Kibe aliwashauri wale ambao tayari wako kwenye ndoa kuwataliki haraka sana wake zao pindi tu wanapoona dalili ya kwanza ya kutaka kuwapoteza.

“Wanaume acha niwashauri, ukiona redflag ya kwanza mrudishe kwao haraka sana, usikuwe kama mimi. Mimi niliona redflag na bado nikaenda kumuoa huyu msichana. Huu ndio muda unatoroka, unaruka upuuzi na unasema wacha tuache. Mwanamke ni kitu hatari sana kwa mwanamume wakati anastahili kuwa kazini,” alisema.

Kibe alisema kuwa uhusiano wa ndoa ni sawa na makalio ya shetani akisema kwamba yeye alishawishiwa kuingia kwenye ndoa kipindi alikuwa mchamungu.

“Nawambia sasa hivi wanaume angalia mbele uone nyota yako, andika chini hiyo ndoto ya maisha yako ya kesho na uone kama kuna mwanamke hapo, huwezi ona,” alimaliza.