logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wacheni kujichora sura yangu-Sonko awaonya wanawake wanaochora tattoo ya uso wake

Alisema alitumia shilingi elfu 5 kuchorwa hiyo tattoo na ni mama kwa watoto wawili.

image
na Radio Jambo

Makala22 August 2023 - 08:35

Muhtasari


  • Jibu la Mike Sonko linakuja wiki moja tu baada ya Maryanne Njoki kutoka Murang'a kujichora tattoo ya uso wake kwenye paja lake.
Aliyekuwa gavana wa Nairoi, Mike Sonko

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko amejibu mwenendo unaokua wa wafuasi kujichora tattoo za uso wake kwenye miili yao.

Haya yanajiri kutokana na kitendo cha hivi majuzi cha Maryanne Njoki cha kuchora tatoo ya uso wa Sonko kwenye paja lake, jambo ambalo lilivuta hisia na kumfanya Sonko atoe mawazo yake kuhusu suala hilo.

Sonko aliingia kwenye mitandao ya kijamii kukiri uaminifu na upendo anaopokea kutoka kwa wafuasi wake huku akieleza kwa upole kutoridhishwa kwake kuhusu chaguo la kuchora tattoo.

"Nafurahia msaada wako wa uaminifu pia mimi nawapenda lakini tafadhali, mimi nitawapenda bila tatoos kwa sababu mwili wako ni wako na bwana wako na wa Mungu," Sonko alisisitiza.

Jibu la Mike Sonko linakuja wiki moja tu baada ya Maryanne Njoki kutoka Murang'a kujichora tattoo ya uso wake kwenye paja lake.

Mrembo huyo aliyefanya mahojiano ya kipekee na ripota wa habari za udaku wa mitandaoni Nicholas Kioko, mrembo huyo aliyejitambulisha kama Maryanne Njoki alisema kwamba aliamua kuchora tattoo kwenye paja lake kwa sababu anampenda tu jinsi anavyosaidia watu.

“Niliamua kuchora ni venye tu nampenda jinsi anavyosaidia watu, nikaona nimchore juu amesaidia watu wengi na sijawahi ona hata mmoja akimrudishia shukrani. Mimi nampenda sana vile anasaidia watu, mimi ni shabiki wake juu yeye hanijui lakini mimi namjua. Nikasema nimchore ndio nikuwe namuona. Nakata nikienda kuoga namuona, nikivaa kaptura fupi namuona,” alisema.

Alisema alitumia shilingi elfu 5 kuchorwa hiyo tattoo na ni mama kwa watoto wawili.

“Mimi hata sikuwa nafikiria kwamba ni kiki natafuta, alinichora tu mimi hata sikupost, jamaa aliyenichora ndio alinipost, hata siko Instagram. Bado sijapatana na Sonko lakini nilikuwa nimesikia aliitisha namba yangu lakini bado hajanipigia.”

“Nikikutana na Sonko nitamwambia nampenda juu anasaidia watu juu sijawahi ona mtu anafanyia watu na pesa zake, mimi chenye naweza kumuambia aendelee tu hivyo na sioni akichoka kwa sababu alianza kitambo na bado anaendelea,” Njoki alisema.

Njoki alisema yeye anafanya kazi ya kuchuuza mboga na matunda huko Murang’a na akikutana na Sonko atamsalimia na hata kumpa kumbato.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved