Agosti 22 amabyo ilikuwa Jumanne, ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya msanii mmiliki wa lebo ya Next Level, Rayvanny.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, mpenzi wake Fahyvanny alimsherehekea kwa ujumbe wenye makopakopa mengi akimuita kama mume wake na kuahidi kuganda kwenye ubavu wake katika miaka mingi ijayo.
Wawili hao walishiriki mfululizo wa picha zao za pamoja wakifurahia siku kubwa kwa bosi huyo wa NLM na mojaya picha ambayo ilinasa macho ya watu ni ile Rayvanny akiwa amemalia makalio ya mpenzi wake.
Hata hivyo, Fahyma aliwazima akiwaambia kukoma tantarira nyingi kwani Rayvanny hajakosea.
"Acha kelele, chui kalala," aliandika.
Katika ile hali ya kutaniana, Fahyvanny alimtaka Rayvanny kuwa muelewa katika ndoa ili kuepusha malumbano ya mara kwa mara, akikiri kwamba ni kweli ana kidomo domo sana lakini kubwa mwisho wa siku ni kumuelewa na kumsamehe.
“Namuomba MUNGU atujaalie na atutimizie kila hitaji la mioyo yetu🙏. Nakuombea mafanikio mengi ktk kazi zako mumewangu, Nakupenda, nakuthamini na kuheshimu pia. Tusameheane pindi tunapokosana Binafsi naomba tu univumilie maana nina mdomo sana,” Fahyvanny alisema.
Alikwenda mbele na kumtahadharisha Rayvanny kwamba kitu ambacho nacho hawezi kuacha kabisa ni kuchakura simu yake ili kuona vipusa wanaommezea baba mtoto wake mate kwenye faragha za mitandao ya kijamii.
“Na kingine mume wangu simu yako kushika siachi hilo ulijue. Nakupenda sana sana kuliko chochote hapa duniani❤️❤️” Fahyvanny aliongeza.
Mwishoni mwa wiki jana, tuliripoti kwamba ilikuwa inakisiwa kuwa na mporomoko katika penzi lao baada ya kubaini kwamba walikuwa wameacha kufuatana katika mitandao ya kijamii.
Lakini kama inavyoonekana ilikuwa ni kama kuwachezea shere mashabiki wao kwani kwa kile ambacho kinaonekana wawili hao wamezama katika kina kirefu sana cha huba.