logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond adai alitumia shilingi milioni 5 kukodisha private jet kutoka New York hadi Detroit

“Halafu sasa kuna ya kuibakisha ilale ili kesho ikurudishe tena,” aliandika Diamond.

image
na Davis Ojiambo

Burudani23 August 2023 - 08:47

Muhtasari


  • • Mwishoni mwa juma lililopita, msanii huyo alionekana kwenye ndege hiyo ya kibinafsi akiwa pamoja na meneja wake Babu Tale na washikaji wake wa karibu.
Diamond

Msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz amefichua kiasi cha hela alizotumia kukodisha ndege ya kibinafasi kumsafirisha kutoka jimbo la New York nchini Marekani hadi jimbo la Michigan kulikokuwa kunafanyika tamasha la Afronation wikendi iliyopita sehemu inayojulikana kama Detroit.

Kupitia Instagram, Diamond alipakia picha ya risiti za kuonesha malipo aliyotoa kwa ajili ya ndege hiyo.

Risiti hizo zilionesha kwamba msanii huyo alizama mfukoni na kutengana na kima cha dola 36800 ambacho ni kiasi sawa na shilingi milioni 5.3 za Kenya kwa ajili tu ya safari hiyo ya mwendo mmoja kutoka New York kwenda Detroit bila kumrudisha.

Diamond kwa tambo nyingi aliandika kwenye picha hiyo ya risiti kwamba ikiwa unashangaa kuhusu kiwango hicho cha juu cha hela, kuna wengine hadi wanalipia gharama ya kuibakisha hadi kesho ili uondoke nayo ikurudishe ilikokutoa.

“Halafu sasa kuna ya kuibakisha ilale ili kesho ikurudishe tena,” aliandika Diamond.

Mwishoni mwa juma lililopita, msanii huyo alionekana kwenye ndege hiyo ya kibinafsi akiwa pamoja na meneja wake Babu Tale na washikaji wake wa karibu.

Kwenye hiyo ndege ya kifahari, walikuwa wameandaliwa vinywaji ghali huku kwenye meza yao kukiwa na kibao cha kuwatambulisha “WCB Wasafi”

Diamond alitumbuiza katika ukumbi wa Afronationa huko Detroit pamoja na wasanii wengine wakiwemo Davido, Burna Boy na wengine kutoka Afrika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved