Ujumbe Mzuri wa Emmy Kosgei kwa Mumewe wanapoadhimisha Miaka 10 kwenye Ndoa

Hakika amefichua kuwa mume amekuwa akimsaidia sana na kumuongezea thamani maishani.

Muhtasari
  • Kosgei ameshiriki ujumbe wa kupendeza kupitia mitandao yake ya kijamii, huku akionyesha upendo wake kwa mumewe.
MSANII EMMY KOSGEI NA MUMEWE
Image: INSTAGRAM

Kosgei ni msanii maarufu wa injili wa Kalenjin.Hata hivyo msanii huyo wa injili na mumewe wa Nigeria wanasherehekea miaka kumi ya ndoa.

Kosgei ameshiriki ujumbe wa kupendeza kupitia mitandao yake ya kijamii, huku akionyesha upendo wake kwa mumewe.

Hakika amefichua kuwa mume amekuwa akimsaidia sana na kumuongezea thamani maishani.

Kosgei amekiri kuwa mumewe amembadilisha tangu wapatane,alipakia picha wakiwa wawili huku akiambatanisha na ujumbe ufuatao;

"Imepita miaka 10 tangu nimfanyie ❤️ mtu huyu wa ajabu mwenye moyo wa dhahabu.. #myhimself my #obim an epitome of upole ❤️ ameongeza thamani sana kwa binti huyu wa kalenjin !! Kukupenda ni rahisi sana ❤️❤️ daima hadi milele ... tunashukuru 🙏 Mungu amekuwa mwaminifu sana 🙏 TUNASHEREHEKEA NEEMA HADI SASA.. haleluya."

Mashabiki waliwatakia maisha mema katika ndoa yao, na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

marychinda: You both are a signage that a Nigerian man can really lead, provide, protect, love and support a woman to the Zenith while she submits,helps his ministry and person.

osei: Happy Anniversary ♥️♥️♥️! We thank God for you both!

kissa: Happiest 10th Anniversary Daddy and Mummy! We pop to many more years of bliss 🥰🇺🇬🇺🇬

cmuneneus: God to continue blessing you both to more blessed years together. Happy 10 years marriage anniversary🙌🙌🙌

felix: Happy anniversary papa and mama, we are thankful to God for you both, may you enjoy eternal bliss now and forever in Jesus name, love you endless