logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bahati amewaacha watu vinywa wazi akiweka picha yake pembeni mwa jeneza

“Hata kama ni wimbo vichekesho vingine ni ghali” Lesley Musili alimwambia.

image
na Radio Jambo

Makala04 September 2023 - 08:47

Muhtasari


• Chapisho hili lenye ukakasi linakuja siku chache tu baada ya msanii huyo kuonekana akiwa studioni kufanya wimbo huku mdomoni anavuta kile kilichotafsiriwa kama bangi.

Bahati na jeneza

Mwanamuziki Staa humu nchini, Bahati Kioko, amewaacha watumizi wa mitandao ya kijamii katika maswali mengi kufuatia chapisho lake jipya kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Bahati alipakia picha ya jeneza na kando yake picha ya sura yake mwenyewe ikiwa imeegemezwa kutoa taswira kwamba picha hiyo ni ya maiti ambayo iko ndani ya jeneza lenyewe la rangi nyeupe.

Msanii huyo japo hakutoa taswira ya moja kwa moja kuhusu ni kipi kinachoendelea katika chapisho hilo, aliandika maneno mafupi tu akiuliza, “Utarudi lini?” na kuifuatisha na emoji za kulia.

Haijafahamika mara moja kama ni project ya wimbo mpya au la lakini picha hiyo imewashtua watu wengi huku wengine wakimtaka aifute kutokana na kwamba haina ujumbe mzuri na haileti maana nzuri kwake.

Haya hapa ni baadhi ya maoni kutoka kwa mashabiki wake;

“Kwani ulikufa bahati wangu,” Mmoja kwa jina Paula aliandika.

“Hata kama ni wimbo vichekesho vingine ni ghali” Lesley Musili alimwambia.

“Anataka kutoa gospel ...Sasa but some clouts ain't necessary Maan...yaan vile watu huogopa kifo ama ni mimi tu maybe💔” Nanish Flora alisema.

“Unacheza na mungu jitabirie tu sun “ Babe Nelly alimwambia.

Chapisho hili lenye ukakasi linakuja siku chache tu baada ya msanii huyo kuonekana akiwa studioni kufanya wimbo huku mdomoni anavuta kile kilichotafsiriwa kama bangi.

Baadhi ya mashabiki walikasirishwa na kitendo hicho wakisema kwamba Bahati – ambaye umaarufu mkubwa aliupata kama msanii wa injili alichokuwa anakifanya ni kama kumkufuru Mungu.

Maoni yako ni yepi kuhusu vitendo vya msanii huyo katika siku za hivi karibuni?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved