Nilijaribu kuwatega wanaume wengi kunipa mimba lakini mimba haikuingia - Lady Risper

" Nilikuwa nadhani mimi ndio tasa siwezi shika mimba. Hatuna nyota ya kushika mimba kwetu, hatukuwa nayo,” Faith alisema.

Muhtasari

• Mrembo huyo alisema hata hivyo kwamba baadae alipata ufunuo kwamba Mungu hakuwa anataka apate mimba kabla ya ndoa.

• Mwezi wa pili baada ya harusi, Faith alisema kwamba alipigwa na butwaa kugundua ana mimba.

Risper FAITH.
Risper FAITH.
Image: Instagram

Mjasiriamali na mwanasosholaiti Lady Risper au ukipenda Risper Faith amefunguka makubwa jinsi alijaribu kutafuta mtoto kwa udi na uvumba lakini njama zote alizojaribu kuzitumia hazikufua dafu.

Akizungumza Jumapili kaitka kipindi cha moja kwa oja kupitia TikTok yake, Lady Risper alikiri kwamba katika maisha yake kabla akutane na mwanaume wake – Brian, alishiriki mapenzi na wanaume wengi sana wa kila rika na umri.

Mrembo huyo alisema kuwa alijaribu kuwaingiza kwenye mtego wanaume hao wote mradi tu apate mimba yao lakini hakufanikiwa, kwa wakati mmoja akadhani kwamba pengine yeye ndiye tatizo.

“Nilikuwa na wababa wengi, nimekuwa na maboufriend wengi, lakini hakuna siku nimewahi shika mimba. Nimejaribu kuwaingiza kwenye mtego wababa wengi sana lakini mimba haijawahi ingia. Nilikuwa nadhani mimi ndio tasa siwezi shika mimba. Hatuna nyota ya kushika mimba kwetu, hatukuwa nayo,” Faith alisema.

Mrembo huyo alisema hata hivyo kwamba baadae alipata ufunuo kwamba Mungu hakuwa anataka apate mimba kabla ya ndoa.

“Lakini Mungu alikuwa anataka niolewe. Nikaolewa na mwezi wa pili baada ya harusi yangu nikapata mimba. Buila kuhangaika. Hata mimi nilishangaa na mtu wa kwanza nilipigia simu ni dadangu. Dadangu hakukubali nikamwambia akaja na vitu vya kupima mimba tukapima mar azote 4 zikaonesha nina mimba,” alisema huku akitokwa na machozi.