logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond kuwafuta wafanyikazi wa Wasafi na mlinzi wake kisa umeme kupotea akitumbuiza

"Ni mara mia mlinzi angesimama mbele ya ya Diamond, ili aendelee kutumbuiza nyuma"

image
na Davis Ojiambo

Burudani05 September 2023 - 07:02

Muhtasari


  • • Wakati wa kutumbuiza kwenye shoo hiyo katika mwendelezo wa tamasha la Wasafi Festival linaloendelea katika mikoa kadhaa nchini Tanzania, umeme ulikatika.
Diamond,

 Mtangazaji wa Wasafi FM na chawa nambari moja wa msanii Diamond Platnumz, Baba Levo amemshauri msanii huyo kuwafuta kazi wafanyikazi wa Wasafi pamoja na mlinzi wake wa kibinafasi baada ya shoo yao ya mkoa wa Mtwara kukumbwa na hitilafu hadi umeme kupotea.

Baba Levo kupitia Instagram yake alisema kwamba kilichotokea katika shoo hiyo ya wikendi kusababisha Diamond kushindwa kutumbuiza ni tatizo la jenereta lililosababishwa na umeme na ambalo lingezuilika mapema.

Baba Levo alisema kwamba Diamond alikwenda hasara kubwa sana kwa kutowatumbuizia watu wa Mtwara mpaka kuridhika, akiahidi kwamba tayari yeye binafsi kama chawa ameanzisha uchunguzi kujua kama tatizo lile kulikuwa na mkono wa mtu au kuzembea kazini.

“Tunachunguza tuone ni nani aliyezembea kazini, au kama ni jenereta lenyewe hakuna shida. Lakini mimi nimemshauri Diamond Platnumz awafukuze kazi watu wanne, kama sio watatu, wengine ni vionozi wa Wasafi media, lakini pia amfukuze baunza au mlinzi wake,” Baba Levo alisema.

Alitetea ushauri huo wa kufutwa kwa baunsa wa Diamond akisema kuwa kitendo cha kumruhusu bosi wake kutumbuiza gizani mbele ya umati bila kumlinda ni kosa la uhaini.

“Kwa kitendo cha kumruhusu Diamond kutumbuiza gizani tena mbele ya umati uliojaa bila kujua kama kuna mtu yeyote anaweza kurusha kitu chochote kibaya kikampata msanii na madhara yakawa mabaya. Ni mara mia mlinzi angesimama mbele ya ya Diamond, ili aendelee kutumbuiza nyuma. Lakini mlinzi alikaa nyuma akamuacha Diamond kama ndiye kiberenge kule mbele anaimba. Haya ni makosa,” Baba Levo alisema akisisitiza kwamba hawawezi kubali makosa ya mlinzi.

Wakati wa kutumbuiza kwenye shoo hiyo katika mwendelezo wa tamasha la Wasafi Festival linaloendelea katika mikoa kadhaa nchini Tanzania, umeme ulikatika na Diamond akalazimika kutumbuiza gizani huku watu wakilalamika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved