Ikatokea Bahati amefariki leo hii, mtu wa kwanza Diana atakimbilia ni mimi - Ringtone

“Mimi nampenda Diana sana na kwa kweli haya leo Bahati – Mungu aipitishe mbali – leo hii afariki asikuwepo, niko na uhakika mtu wa kwanza ambaye Diana atamkimbilia kumwambia ndugu yako hayuko ni mimi."

Muhtasari

• Msanii huyo alisema kwamba kile kinachodhaniwa na mashabiki kuwa ni chuki ni kukosoana tu katika baadhi ya vitu ambavyo havifanyiki kwa njia sahihi tu basi.

Bahati na mkewe, Ringtone
Bahati na mkewe, Ringtone
Image: Instagram

Msanii wa injili Ringtone Apoko amefichua sababu ya kusimama upande wa kumkingina kifua Diana Marua baada ya kuzomwa mitandaoni kutokana na vazi ambalo alikuwa amelivaa wiki chache nyuma wakati wa kupiga picha ya mtoto wake wa kufikia, Morgan Bahati.

 Akizungumza na Mungai Eve, Ringtone alisema kwamba kilichomfanya kusimama na Diana ni kwa sababu aliona vibaya watu kumvuta mtoto asiye na hatia kwenye zogo hilo, wakianza kusema kwamba Morgan alikuwa anafanana na mwanasoka Victor Wanyama.

Cha pili ambacho kilimfanya Ringtone kumtetea Diana Marua ni kwa sababu alisema kwamba anampenda sana Zaidi ya mipaka.

Ringtone alifanya kufuru kwa kutaja kwamba ikatokea leo hii mumwe Diana Marua, Bahati Kioko akafa, mtu wa kwanza ambaye Diana atakimbilia si mwingine bali ni yeye, akiwataka Wakenya kuacha kuchanganyikiwa na kudhani kwamba wao ni maadui.

“Mimi nampenda Diana sana na kwa kweli haya leo Bahati – Mungu aipitishe mbali – leo hii afariki asikuwepo, niko na uhakika mtu wa kwanza ambaye Diana atamkimbilia kumwambia ndugu yako hayuko ni mimi. Uliza Diana, siku moja muulize, wanajua kwamba kaka mkubwa wa Bahati ni mimi. Vita vyetu vya huku nje havimaanishi chochote, tunapendana sana,” Ringtone alisema.

Msanii huyo alisema kwamba kile kinachodhaniwa na mashabiki kuwa ni chuki ni kukosoana tu katika baadhi ya vitu ambavyo havifanyiki kwa njia sahihi tu basi.

“Tunakosoana tu, venye nimesema kuwa Bahati anavuta bangi, si eti nimemchukia, nataka watoto na wale wasanii wanaokuja kuelewa kwamba kuna vitu hatuwezi fanya, sisi ni kioo cha jamii."

Ringtone alikosoa Watu kujaribu kumuingiza mtoto Morgan kwenye zogo la kumzomea Diana wakimhusisha mtoto huyo kuwa tunda la kutokana uhusiano wa awali wa Marua na Wanyama.