Mwanablogu Nicholas Kioko awatambulisha wanawe mapacha kwa mashabiki wake

“Mapacha ni baraka kutoka kwa Mungu. Wao pia ni wa ajabu sana. Kutana mapacha wetu hatimaye,” wapenzi hao waliandika katika chapisho la pamoja Instagram.

Muhtasari

• Mwanzoni mwa Desemba mwaka jana, Kioko na Wambo waliandaa sherehe ya kufichua ujauzito kwa kushirikiana na hospitali ya Komarock.

Nicholas Kioko na mapacha wake
Nicholas Kioko na mapacha wake
Image: Instagram

Mwandishi wa habari za mitandaoni Nicholas Kioko na mpenzi wake Wambo Ashley kwa mara ya kwanza wamewatambulisha wanao mapacha wa kiume kwa mashabiki wao mitandaoni.

Kioko na Ashley walibarikiwa na mapacha hao wa kiume, Roman Reigns na Roman Leo takribani miezi 7 iliyopita na hii ndio mara ya kwanza kabisa wanaonesha sura zao kwa mashabiki wao katika mitandao ya kijamii.

“Mapacha ni baraka kutoka kwa Mungu. Wao pia ni wa ajabu sana. Kutana mapacha wetu hatimaye,” wapenzi hao waliandika katika chapisho la pamoja Instagram.

mapacha wa Kioko
mapacha wa Kioko

Wapenzi hao miezi kadhaa iliyopita wakati wa kutangaza kuwa wanatarajia mapacha wote wa kiyume, waliandaa tafrija la aina yake lililohudhuriwa na marafiki wao wa karibu ambapo walitangaza habari hizo njema.

Hafla hiyo ya utambulisho wa jinsia ya watoto wao, wanablogu mbalimbali walihudhuria kuwapa shavu na kongole kwa hatua hiyo yenye kheri katika maisha ya wapenzi.

Kioko alimshukuru Mungu kwa kumpa Baraka hizo huku akisema anajihisi mwenye fahari kushuhudia safari yake akivuka kutoka ujanani hadi kuwa mzazi mtarajiwa.

“Asante Bwana kwa kutimiza ndoto zetu. Sisi sote hatuwezi kungoja kuwashikilia wavulana wetu hivi karibuni,” Kioko aliandika Instagram.

Mwanzoni mwa Desemba mwaka jana, Kioko na Wambo waliandaa sherehe ya kufichua ujauzito kwa kushirikiana na hospitali ya Komarock.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kioko alipakia picha maridadi pamoja na kionjo cha video ya jinsi walifichua ujauzito wao na kusema kuwa ni Baraka kuwa na furaha kuwa ni baba mtarajiwa tena wa mapacha.

“Mioyo yetu imejaa🙏 Miale miwili midogo ya jua kutoka kwa Mungu. Tunayo furaha kuwatangazia kuwa tunatarajia mapacha. Tutashiriki safari yetu na nyinyi ....Mungu ni Mwema,” Nicholas Kioko alisema.

Wanandoa hao ambao wanajulikana kwa video zao za kusisimua za YouTube walikuwa wametania habari hizo kwa muda na kusababisha mashabiki kudhani baada ya kutangaza kuwa walikuwa na habari kubwa za kushiriki.