Christiano Ronaldo akiri kuwa mara kwa mara huwa anajitafuta kwenye google

Ronaldo mwenye umri wa miaka 38 alikiri kucheza soka lake hadi miaka 40 na pia alikiri kwamba huwa anakula vyakula vya kuchuuzwa mitaani.

Muhtasari

• “Ndio nimewahi jitafuta mara nyingi tu,” Ronaldo alijibu na kifaa hicho cha kugundua uongo na ukweli kikakubaliana na jibu lake.

 
• Mchezaji huyo pia alikiri kwamba yeye mara nyingi hula vyakula vya mtaani.

Ronaldo
Ronaldo
Image: Instagram

Siku moja iliyopita, mchezaji namba moja duniani kwa muda wote Christiano Ronaldo alikuwa gumzo la mitandaoni baada ya shirika la biashara za fedha Binance kufichua mahojiano waliyofanya na mchezaji huyo nguli kutoka Ureno.

Ronaldo kwa muda sasa amekuwa balozi wa mauzo wa kampuni hiyo na safari hii waliamua kumweka kwenye kiti moto wamtaka kujibu maswali yao moja kwa moja kwa kutumia ndio au hapana bila kujieleza kisha wanaweka jibu lake kwenye mtandao wa kugundua uongo na ukweli.

Katika moja ya maswali, mhoji Andy alimuuliza iwapo amewahi jitafuta kwenye mtandao mkuu wa kutafuta vitu mbali mbali wa Google.

“Ndio nimewahi jitafuta mara nyingi tu,” Ronaldo alijibu na kifaa hicho cha kugundua uongo na ukweli kikakubaliana na jibu lake.

Mchezaji huyo pia alikiri kwamba yeye mara nyingi hula vyakula vya mtaani.

Ronaldo alikiri pia kwamba ligi kuu ya premia nchini Uingereza ni moja ya ligi ngumu Zaidi duniani, jibu ambalo lilikuwa kweli kulingana na kifaa cha kugundua uongo na ukweli.

Nahodha huyo wa Ureno ambaye kwa sasa ni wa moto kuiwajibikia timu ya Al Nassr ya Saudi Arabia alisema kwa kusisitiza kwamba analenga kucheza soka hadi pale atakapofikisha umri wa miaka 40.

Ronaldo kwa sasa yuko na umri wa miaka 38.