logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nikomeni!Matubia asema huku akikanusha madai kuwa amerudiana na Ex wake Lung'aho

Maoni mengi yalisema kwamba hii ilikuwa mikono ya Jackie

image

Burudani06 September 2023 - 15:00

Muhtasari


  • Huku akijibu na kukana madai hayo,Jackie alionekana kukejeli maua ambayo ex wake alikuwa ameshika.

Mwigizaji wa Kenya Jackie Matubia ametumia mtandao wake wa Instagram kukanusha madai kuwa yeye na mpenzi wake wa zamani wamerudiana.

Mapema leo ex na baba mtoto wake  Blessing Lung'aho walishiriki picha na mwanamke asiyejulikana na mawazo yalifanywa kuwa anaweza kuwa Jackie Matubia.

Katika picha hiyo, Blessing alikuwa ameshika chombo cha maua na kitu pekee kilichoonekana kwa bibi huyo ni mikono yake tu tangu afikishe macho yake.

Maoni mengi yalisema kwamba hii ilikuwa mikono ya Jackie na ilivutia umakini wake na aliishughulikia kwa njia bora zaidi.

Huku akijibu na kukana madai hayo,Jackie alionekana kukejeli maua ambayo ex wake alikuwa ameshika.

Pia alisema kuwa hajawahi fanya maudhui mabaya na hawezi kwa hivyo watu wanapaswa kumkoma.

"Iwafikie, unaweza kulinganisha kucha hizi na hizo tafadhali. Sijihusishi na maudhui ya Mbaya, Nikomeni," aliandika kwenye stori zake za Insta.

Mwigizaji na mwigizaji wa Salem Blessing Lung'aho walitengana miezi michache baada ya kumkaribisha mtoto wao wa kwanza pamoja.

Haijabainika ni kwa nini wawili hao waliachana lakini ni wazi kuwa huenda wasirudiane tena wakiwa wanandoa.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved