Amber Ray ajigamba baada ya mpenziwe kumfanyia 'shopping' ya shilingi 158K - Video

“Pata mwanamume ambaye ni mchanga vya kutosha kuburudisha, mwenye umri wa kutosha kuongoza, mwenye nguvu za kutosha, nduli wa kutosha kulinda na kukomaa vya kutosha piga hatua."

Muhtasari

• Baada ya kulipa, Amber Ray alionesha kiasi cha pesa ambacho Rapudo alitengana nacho kutoka katika kadi yake ya ATM kwa ajili ya vyakula hivyo.

Rapudo na mkewe Ray.
Rapudo na mkewe Ray.
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Amber Ray ambaye amejipa jina la kimajazi kama Bibi wa Tajiri ni mmoja kati ya wanawake wachache ambao wanaishi maisha ya kweli katika ndoa.

Hii ni baada ya mrembo huyo mama wa watoto wawili kuonesha jinsi waliandamana na mumewe Kennedy Rapudo hadi katika duka kuu na kufanya ununuzi wa vyakula kwa Zaidi ya laki moja pesa za Kenya.

Rapudo ambaye hajawahi weka wazi chanzo cha utajiri wake amekuwa akimrembesha Amber Ray na zawadi ghali na ainati tangu atangaze kwamba amepata mimba yake na hata kumzalia mtoto wa kike, Afrikana.

Katika video ambayo mrembo huyo alipakia katika ukurasa wake wa Instagram, walionekana wamepiga foleni katika duka kuu wakielekea kulipa huku wamenunua shehena ya vyakula mbali mbali.

Baada ya kulipa, Amber Ray alionesha kiasi cha pesa ambacho Rapudo alitengana nacho kutoka katika kadi yake ya ATM kwa ajili ya vyakula hivyo.

Ray alijigamba katika video hiyo akimshukuru Rapudo kwa kuwa mume na baba bora kwa wanawe ambaye siku zote si mkono birika ikija ni katika masuala ya kutumia pesa kwa wale awapendao.

“Pata mwanamume ambaye ni mchanga vya kutosha kuburudisha, mwenye umri wa kutosha kuongoza, mwenye nguvu za kutosha, nduli wa kutosha kulinda na kukomaa vya kutosha piga hatua😉. #Bibiyatajiri #endmonthshopping🛒 .... @99martkenya tulipenda sana huduma yako,Asante.😇” Ray aliandika kwa majigambo ya kiwango cha juu.

Haya hapa ni baadhi ya maoni kutoka kwa mashabiki wake;

“Caption tuu 🙌🙌. @kennedyrapudo we are solly 🙌🏽🙌🏽. Inshallah Mtu ntapata aweke caption Kama hii nampea password ya Kila kitu maishani 😹😹😹😹” Ian Musili alisema.

“Ni kaharabu na Regina Daniels pekee wanaoweza kunishauri,” mwingine alisema.