logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mr Seed ajibu dai la Xtian Dela kuwa wakati wa ajali walikuwa walevi, "Walitaka tufe wote!"

Aidha alisema aliumizwa sana na madai ya Dela lakini akashikilia kuwa hawezi kumtakia mabaya.

image
na Radio Jambo

Makala08 September 2023 - 10:41

Muhtasari


• Seed alisema kwamba matamshi ya Dela yalimfanyaq kuhisi kwamba baadhi ya watu walichukulia nafasi hiyo kuomba kwamba wangeangamia wote katika ajali hiyo.

• Wakati wa ajali, Seed alikuwa na marafiki zake wa karibu akiwemo marehemu Ambroze Khan na msanii mwenza katika injili DK Kwenye Beat.

Xtian Dela na Mr Seed.

Msanii wa humu Nchini Mr Seed kwa mara ya kwanza baada ya miezi minne, amevunja kimya kuhusu ajali mbaya ya barabarani aliyopata pamoja na marafiki zake mwezi Aprili kupelekea kufariki kwa mpiga picha wake.

Seed, katika mahojiano na mwanablogu wa habari za mitandaoni Eve Mungai, alisema kwamba mwanablogu na mtangazaji Xtian Dela alimuumiza sana hisia zake katika matamshi ambayo alitoa kipindi hicho kuhusu ajali yenyewe.

Xtian Dela alidai kuwa wasanii hao walikuwa wakiendesha gari wakiwa wamelewa na aliwalaumu kwa kifo cha Ambroze. Alizitaka mamlaka kuwachunguza na kubaini chanzo halisi cha kifo hicho.

Seed alisema kwamba matamshi ya Dela yalimfanyaq kuhisi kwamba baadhi ya watu walichukulia nafasi hiyo kuomba kwamba wangeangamia wote katika ajali hiyo.

Wakati wa ajali, Seed alikuwa na marafiki zake wa karibu akiwemo marehemu Ambroze Khan na msanii mwenza katika injili DK Kwenye Beat.

“Kulikuwa na wenye wanawish sisi wote tungededi. Nilikuwa naskia juu hio kipindi nilikuwa nimetoka social media. Maswali mbona huyu bwana hivi mbona hamkufa wote. Ajali si ati ni kitu tumepangia. Mungu si fala wale watu wanapangia watu mabaya hao ndio huend up…sa imagine ati tumepanga for what benefit, for what reasons it was crazy,” aliambia Mungai Eve.

Aliongeza kuwa wote waliokuwa kwenye gari hilo hawanywi pombe. Msanii huyo wa zamani wa injili pia alishangaa kwa nini Dela hakuwepo kwenye mazishi ya Ambroze baada ya kudai kuwa alikuwa rafiki yake.

“Hakuna mtu alikuwa mlevi, huwezi kupanga ajali na narespect opinion ya kila mtu lakini kama yeye [Dela] anasema alikuwa rafiki yake [Ambroze] mbona hakuenda hio mazishi hata hiyo service ilikua kwa church. Kazi yake ilikuwa ni kutuwish vibaya mtandaoni. Hio time nilikuwa kwa situation mbaya sana, nilikuwa kwa depression imagine kukaa kwa kitanda same position wife alikuwa ananiosha literally halafu bado namourn beshte yangu mwenye nimespend na yeye the who day halafu inafika hayuko then you because uko na power kuwa influential,” Mr Seed aliongeza kwa kutamauka.

Aidha alisema aliumizwa sana na madai ya Dela lakini akashikilia kuwa hawezi kumtakia mabaya.

“Binafsi naweza ambia Xtian alinihurt feelings, sijawahi crossian naye popote. Tulikuwa tuanapata tukianza hapo system unit. Aliniattack time niko situation mbaya sana na hio hajui kitu effect ilimake kwa watu. Niiskia vibaya sana yeye mweneyewe siwezimuishia kitu mabay nashukuru Mungu niliovercome, nilimuomba Mungu juu ya hali nzima, bado naomboleza Ambro hadi leo huyo ni kaka yangu,” alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved