Kapkeno, shabiki wa Manchester United humu nchini ambaye alifanya kufuru kwa kula mayai Zaidi ya 15 ili tu kuheshimu makubaliano ya bet hatimaye amezungumza na ametuma ujumbe kwa timu hiyo akiomba msaada.
Kapkeno kuelekea mechi ya wikendi jana kati ya watani wa jadi katika soka la ligi kuu ya Uingereza, EPL – Arsenal na Manchester United, alikuwa ameandika bango akiahidi mashabiki wa timu zote mbili kwamba endapo United ingeshindwa, alikuwa tayari kula mayai 15.
Baadae matokeo yalikamilika kwa Arsenal kuinyuka United katika uga wao wa nyumbani – Emirates – kibano cha mabao 3-1 na hivyo kumweka Kapkeno chini ya shinikizo katika kutekeleza ahadi yake.
Kweli kwa maneno yake, alikula mayao hayo ambayo baadae yalimfurisha tumbo kupelekea kulazwa.
Na baada ya kuondoka hospitalini, Kapkeno sasa anaitaka timu ya Manchester United kumpa msaada wa kufadhili tikiti yake ya ndege kuelekea ugani Old Trafford lakini pia tikiti ya kutazama mechi moja kwa moja katika uwanja huo wa kihistoria kama njia moja ya kumfajiri kwa ushabiki wake kindakindaki kwa The Red Devils.
“Mpendwa Man United, nilikula mayai baada ya kuahidi kufanya hivyo kwa mashabiki wangu kwamba ikiwa Arsenal ingetushinda. Kwa bahati nzuri niko hai baada ya kulazwa hospitalini. Tafadhali niruhusu kuutazama mchezo wa moja kwa moja uwanjani Old Trafford. Mitajihisi vizuri sana,” Kapkeno aliandika katika bango lingine.
Kapkeno alikuwa ameonyesha imani kubwa kuwa klabu yake anayoipenda zaidi ya Manchester United ingeshinda dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Emirates Jumapili iliyopita na hata akaapa kula mayai 30.
Msanii huyo kutoka Eldoret baadaye alijaribu kutimiza ahadi yake huku marafiki zake wawili wakitazama na kupeperusha tukio zima moja kwa moja kwenye mtandao wa Facebook. Hata hivyo, alipokuwa amekula nusu ya trei, alionekana kupata matatizo na akazimia.