Akothee awajibu wanaotaka kujua aliko mume wake Mr Omosh

” Kwa nini niweke maisha yangu ya mapenzi kwa ajili yako? Je, huna chako cha kutazama, tuliachana kitambo sanaaaaa,” Akothee alimjibu shombo shabiki huyo.

Muhtasari

• Kwenye chapisho hilo hilo Akothee ambaye aliwahi kufichua kuwa hawezi kuolewa kwa ajili ya mali.

wakifurahia fungate jijini Santorini, Ugiriki.
Akothee na mumewe Denis Shweizer wakifurahia fungate jijini Santorini, Ugiriki.
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Msanii wa kizazi kipya na mjasiriamali Akothee ambaye baada ya harusi yake kuu alianza kujirejelea Bi Schweizer kwa mara nyingine tena amewafunga mashabiki kwa kuuliza aliko mumewe Omosh.

Kwenye chapisho la Instagram ambapo Akothee alikuwa akitoa mawazo yake kuhusu jinsi watu tofauti wanavyopenda kuhusiana na hali yao ya kifedha mashabiki wake walichukua fursa hiyo kuuliza mwanaaume wake alikuwa wapi licha ya yeye kusema wakati mwingine hatachapisha moja kwa moja kuhusu mapenzi yake.

"Tafadhali Omoshi yuko wapi tulikukosa nyinyi wote wawili tumekuwa tukionana peke yetu Uswizi tafadhali tutafurahi kukuona pamoja ambapo Mr Omoshi ni kawaida kwani tulikufahamu vyema hukuwahi kumpost tangu muda mrefu sana madam Akothee"

” Kwa nini niweke maisha yangu ya mapenzi kwa ajili yako? Je, huna chako cha kutazama, tuliachana kitambo sanaaaaa,” Akothee alimjibu shombo shabiki huyo.

Kwenye chapisho hilo hilo Akothee ambaye aliwahi kufichua kuwa hawezi kuolewa kwa ajili ya mali alisema kuwa wanawake wenye utoshelezaji wa kifedha ni wa kweli linapokuja suala la mapenzi ikilinganishwa na wale ambao hawana pesa.

"Usimpe mwanamke hisia kuwa una pesa wakati hupendi tu wanawake usijaribu kudanganya punda ambao hawana 🤣🤣🤣🤣🤣 Ninapenda kusimamia matarajio ya watu kabla ya kukata tamaa 🤣🤣 Mwanamke ambaye ana pesa zake atakupenda kwa ajili yako , Mke atafanya maamuzi ya kukupenda kutokana na njaa na bili zake 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣. Kuwa wewe ili usipoteze zote mbili 💃🤣🤣"