logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Charlene, Binti wa rais Ruto afurahia kufuzu astashahada baada ya kozi ya miezi 3

Mrembo huyo alidokeza kwamba tayari amejisajili katika ngazi ya juu katika masomo ya lugha za ishara.

image
na Radio Jambo

Makala11 September 2023 - 03:54

Muhtasari


• Charlene Ruto alidokeza kwamab alikuwa ameshiriki masomo hayo kwa kipindi cha miezi mitatu.

Charlene Ruto

Binti wa kwanza wa taifa Charlene Ruto ni mwenye furaha baada ya kufuzu kwa masomo ya astashahada katika kitivo cha lugha ya ishara.

Binti Ruto kupitia ukurasa wake rasmi wa X, awai ukijulikana kama Twitter alipakia msururu wa picha akiwa ameangaza kwa tabasamu pana katika panda la uso huku akiwa ameshika maua kama ishara ya kushereheka.

Charlene Ruto alidokeza kwamab alikuwa ameshiriki masomo hayo kwa kipindi cha miezi mitatu.

“Baada ya miezi 3 ya kusoma Lugha ya Ishara ya Kenya (maarufu kama KSL) kama kozi ya msingi, hatimaye nilihitimu na cheti changu!” alisema.

“Sikuweza kujivunia zaidi yangu! Nilipokutana na Babelyn Mukila mapema mwaka huu na aliwasiliana nami kupitia KSL pekee na ilizua shauku yangu si tu katika lugha bali zaidi kwa vijana Viziwi, jumuiya ya Viziwi na utamaduni wa Viziwi. Nimekuja kukuza shauku na upendo kama huu kwa Viziwi,” aliongeza binti Ruto.

Mrembo huyo mwenye jitihada katika masuala mbali mbali alisema kwamba kujifunza kozi ya kuwasiliana na viziwi ilimpa nafasi ya kufungua wigo wa fikira zake jambo ambalo hakuwa analitarajia.

“Kujifunza KSL kulifanya sehemu ya ubongo wangu ambayo sikuwahi kujua nilikuwa nayo hapo awali, ilijaribu uvumilivu wangu na nidhamu na kuninyoosha,” alisema.

Aliwashukuru walimu wote waliohakikisha muda wake wa miezi mitatu katika kozi hiyo haukumfanya kujutia huku akiwataja kwa majina.

“Shukrani zangu za dhati kwa Youla Nzale, kwa kuniandalia masomo yangu, mwalimu wangu Rosemary Indeche aliyenifundisha kwa uvumilivu kama huu, Mtahini wangu Washington Akaranga, Leakey Nyabaro, @NickTolina, @BabelynnMukila, Baraza Joseph, Benson Kariuki na Vijana wengine wengi Viziwi ambao mara kwa mara walinisaidia kufanya mazoezi,” alishukuru.

Mrembo huyo alidokeza kwamba tayari amejisajili katika ngazi ya juu katika masomo ya lugha za ishara.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved