Diana Marua amlazimisha Bahati kumuonesha kuwa alim'miss baada ya kurejea nyumbani

“Usinifanye niwe na maswali katika akili yangu, umenimiss? Basi nionyeshe kwamba umeni’miss. Nionyeshe. Usiniambie kwamba umechoka, hata mimi nimechoka,” Diana alimuamuru Bahati.

Muhtasari

• Jambo hilo lilimuudhi Diana ambaye kwa ukali alimshrutisha Bahati kumuonesha jinsi gani amemkosa tangu alipotoka nyumbani na kurudi.

Diana Marua na Bahati.
Diana Marua na Bahati.
Image: Screengrab

Msanii ambaye pia ni mwanablogu wa YouTube Diana Marua amepakia klipu fupi ya kuonesha jinsi anavyompokea mumewe Baahti nyumbani kila anaporejea baada ya mitikasi ya siku.

Katika klipu hiyo, Diana alionekana anatoka ndani ya nyumba akiulizia alipo mume wake hadi pale alipomkuta nje ameketi kwa hali ya kuchoka.

Diana moja kwa moja alimrukia mapajani na kumkalia huku akimkosha kwa mabusu ya moto lakini muda huu wote Bahati alionekana kutoakuwa na mbwembwe huku akisisitiza kwamba alikuwa amechoka.

Jambo hilo lilimuudhi Diana ambaye kwa ukali alimshrutisha Bahati kumuonesha jinsi gani amemkosa tangu alipotoka nyumbani na kurudi.

“Usinifanye niwe na maswali katika akili yangu, umenimiss? Basi nionyeshe kwamba umeni’miss. Nionyeshe. Usiniambie kwamba umechoka, hata mimi nimechoka. Hebu simama na unioneshe kwamba umeni’miss,” Diana alimwambia kwa kumuamrisha huku akisimama.

Bahati bila kuwa na mbadala ya cha kufanya, alisimama na kumkumbatia mpenzi wake kabla ya wawili hao kuingia kwa nyumba.

Bahati na Diana wamekuwa wakioneshana mapenzi bayana bila kuogopa nini ulimwengu utasema kuwahusu.

Kwa mara nyingi, baadhi ya wanaoonea gere mapenzi yao wanadai kwamba Diana anamtawala mpenzi wake kwa jinsi anavyomuamrisha kufanya vitu na Bahati kufanya japo kwa kile kinachoonekana kama ni shingo upande.