Mr Seed asimulia jinsi alivyonusurika kimiujiza kwenye ajali barabarani

Msanii huyo amekiri kuwa hali yake haijakuwa sawa kabisa kwani hawezi kusimama kwa muda mrefu

Muhtasari

•mwimbaji huyo pamoja na wengine watano walihusika katika ajali ya barabarani ambayo ilipelekea wenzake watatu kufariki.

•"Ilikua crazy time for me, na wakati mwingine nlikua dipressed na nlikua naona kama sitawahi tembea,"

Mr Seed ahusika katika ajali mbaya ya barabarani.
Mr Seed ahusika katika ajali mbaya ya barabarani.
Image: Instagram

 

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Mr seed amefunguka kuhusu hali yake baada ya kuhusika kwenye ajali mbaya miezi mitatu iliyopita.

Katika mahojiano na Mungai Eve, Mr Seed aliwashukuru mashabiki wake kwa kusimama naye katika kipindi hicho kimgumu akisema kupitia kwa maombi ameweza kupata nafuu.

Anasema hali ilikua ngumu kwake baada ya kuarifiwa na daktari kuwa amevunjika mfupa wa mguu na kukata tamaa kuwa hangeweza kutembea tena;

"Ilikua crazy time for me, na wakati mwingine nilikuwa depressed na nlikuwa naona kama sitawahi tembea,"

Ajali hiyo iliyotokea eneo la Chaka, ilihusisha gari la G-tours iliyogongana na gari waliyokuwa wakitumia na wenzake walipokuwa wakielekea kufanya shughuli za usanii.

Mr Seed hakuamini macho yake kuona kwamba yuko hai na alizimia kwa zaidi ya dakika ishirini.

Baadaye, walipata usaidizi kutoka kwa abiria walioona ajali hiyo. Seed anasema, abiria hao walitoa huduma za haraka baada ya kumtambua yeye na wenzake na kuwakimbiza hospitalini.

Ameeleza kuwa Dereva wa gari walilokuwa wanatumia , alifariki njiani akipelekwa kupokea matibabu Kaunti ya Nyeri.

Aidha amesema kuwa akipiga kisengere nyuma jinsi hali ilikuwa kwenye ajali hiyo anaathirika kimawazo

Alieleza kuwa alipokea taarifa za kuvunja moyo kwenye mitandao, kwa madai ya kulaumiwa kuwa  yeye pamoja na wenzake  walikua walevi, madai ambayo ameyakana na kubainisha kuwa hatumii vinywaji vikali.

Msanii huyo amekiri kuwa hali yake ingali bado haijarejea sawa kwani bado hawezi kusimama kwenye jukwaa kwa muda mrefu sababu ya maumivu.

Kulingana na yeye,hali yake imechangiwa na ushawishi mkubwa kutoka kwa marafiki, na familia hasa mkewe na wanaye.

Mnamo Aprili 29, mwimbaji huyo pamoja na wengine watano walihusika katika ajali ya barabarani ambayo ilipelekea rafiki yake mmoja kufariki.

Kupitia ujumbe aliochapisha kwenye kurasa za mitandao, Seed alisema, haijawa rahisi kwake kutembea;

"Siku 25 kwenye kitanda hiki sikuweza kutembea au kujisafisha baada ya ajali, inakatisha moyo,"

Mr seed aliwaomba mashabiki wake wamkumbuke kwa maombi akionyesha matumaini kuwa atapona;

"Endelea kuniombea, nitasimama tena,"