Katika hali ya kushangaza, mchungaji Ezekiel Odero ameibuka na ushauri kwa wanaotarajia kuoa huku akishauri wanaume dhidi ya kuoa mrembo yeyote mwenye jina la Diana.
Katika klipu hiyo ambayo imeenezwa mitandaoni, mchungaji huyo alianza kuuliza waumini wake kama wamewahi shuhudia mwanamke yeyote mwenye jina Diana akiwa kwenye ndoa.
Ezekiel alisema kuwa iwapo mwanamke kwa jina Diana atafanikiwa kuwa kwenye ndoa, basi ndoa hiyo moja kwa moja huwa inaongozwa na yeye huku mwanamume akilazimika kufuata masharti yake kama ambavyo maji yanafuata mkondo.
“Umeshawahi kuona Diana yeyote kwa ndoa? Hakuna hata mmoja hivi. Ukioa Diana uishi na yeye, yeye ndiye anakuongoza kama robot anakubeba hivi, utaishi na Diana, anakuwa mwanamume. Lakini wewe uwe mume, Diana anaenda. Hapo nimeongea ukweli,” Pasta Ezekiel alisema.
Jambo la pili ambalo aliwashauri waumini wake ni kukoma kuwapa wanao majina ya Diana akisema ni majina yenye historia isiyo nyooka.
“Usimpe mtoto wako jina Diana, sababu akiolewa, utamshare na watu, Diana anapendwa bila sababu hata kama hajui. Bila yeye kujua, mtu anamwambia nikikwangalia akili inachanganyikiwa, kwa sababu jina hilo linabeba roho mbaya,” Ezekiel alisema.
Tazama video hii hapa chini utoe maoni yako;