Burna Boy atishia kuacha muziki, adai mapato yake hayajaongezeka kwa miaka 3

Hata hivyo, alisema kuwa huenda akachukua mikakati ya kufuata nyayo za msanii Rihanna na kurudi kwa kishindo katika ubora wa kimapato katika muziki.

Muhtasari

• Katika mwaka wa 2022 kuelekea mwaka huu wa 2023 aliingiza Zaidi ya dola milioni 300.

Burna Boy
Burna Boy
Image: Insta

Msanii namba moja wa muziki wa Afrobeats Burna Boy ametishia kwamba huenda akalazimika kuacha masuala ya muziki akitaja biashara ya muziki kuwa ngumu kwa upande wake kwa mapato duni.

Kupitia Instagram Story yake, Burna Boy aliandika akisema kuwa katika kipindi kifupi kijacho atalazimika kuketi na kupiga tathmini kuhusu maisha yake ya kimuziki na iwapo hatoona dalili yoyote chanya basi huenda akalazimika kubwaga manyanga.

“Kwa takwimu ambazo ninaziona kwenye mkataba huu, hii miaka ijayo ya taaluma yangu kimuziki nafikiri iko karibu kunionesha ikiwa kweli napenda kufanya muziki. Mungu pengine anataka kwa kweli kunijaribu ikiwa napenda muziki,” Burna Boy aliandika.

Hata hivyo, alisema kuwa huenda akachukua mikakati ya kufuata nyayo za msanii Rihanna na kurudi kwa kishindo katika ubora wa kimapato katika muziki.

“Hata huenda nitarudi kwa kishindo kwenu nyinyi wote kama Rihanna,” aliongeza.

Kwa mujibu wa majaribu wa majarida ya Marekani ambayo yanafuatilia kwa ukaribu mitikasi ya wasanii wa Kiafrika, Burna Boy aliwahi nukuliwa akilalama kuwa japo anafanya vizuri lakini kiasi cha fedha ambacho anakipata kutoka kwa maokoto ya usambazwaji wa miziki yake ni cha kiwango cha chini.

Katika mwaka wa 2022 kuelekea mwaka huu wa 2023 aliingiza Zaidi ya dola milioni 300 lakini ilielezwa kwamba katika kipindi cha miaka 3 mfululizo, utajiri wake haujawahi kuongezeka hata kwa asilimia moja.