logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nameless, Wahu kushiriki hadithi 18 za uongo kuhusu ndoa walizojifunza miaka 18 ya ndoa

Wawili hao wamekuwa kwenye ndoa kwa kipindi cha miaka 18.

image
na Radio Jambo

Habari12 September 2023 - 08:29

Muhtasari


• Kabla ya kuoana rasmi mwaka 2005, walidokeza kwamba walikuwa wamechumbiana kwa miaka 8.

Nameless na Wahu

Familia ya maceleb, Nameless na Wahu wiki hii wanasherehekea miaka 18 tangu walipofunga harusi mwaka 2005.

Wasanii hao wawili ambao wanatajwa kuwa kielelezo bora kwa jamii si tu katika muziki bali pia katika masiha yao ya ndoa na familia kwa jumla sasa wamedokeza kwamba hivi karibuni watakuwa wanashiriki hadithi 18 za kupotosha kuhusu ndoa ambazo wamejifunza katika safari yao ya miaka 18 kuwa si za kweli.

Nameless kupitia kurasa zake mitandaoni alianza kwa kuwashukuru wafuasi na mashabiki wao waliowaandikia jumbe za kheri njema tangu wikendi na kusema kwamba wamezisoma zote japo hawawezi kuzijibu zote kwa sababu ya muda.

Aliweka wazi kwamba watakuwa wanashiriki hadithi hizo za kupotosha kuhusu ndoa kama njia moja ya kuwatia moyo mashabiki wao walioko katika ndoa na wale ambao wanafikiria kuingia katika ndoa.

“Fam, wazito, wadau,😊 asante kwa jumbe zote za moyo za pongezi kwa Maadhimisho haya ya Miaka 18 ya ndoa yetu! 🙏🏿🙏🏿♥️tumezisoma, 🙏🏿 TunawaAppretiate 🙏🏿🙏🏿... Halafu, Tunafikiria kushirikisha hadithi 18 za ndoa ambazo tumegundua kupitia miaka 18 ya ndoa kuwa sio za kweli. ️🤦🏾️saidia wengine 😁” Nameless aliandika.

Kwa upande wa mkewe Wahu, alipakia kipande cha video Jumatatu na kuwataarifu mashabiki wao kwamba walikuwa wamefunga safari kwenda sehemu ambayo hata hivyo hawakutaja wakisema kuwa wanaenda kusherehekea miaka 18 katika ndoa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved