• Billnass ameyasema haya kukiwa ni miezi kadhaa baada ya kugonga vichwa vya habari alipotambulisha wazi penzi lake na Nandy.
Mjasiriamali wa bidhaa za kielektroniki Nengatronics ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva Billnass amezua mjadala baada ya kutoa maoni kwamba kuna tofauti kati ya matajiri na maskini katika suala zima la mapenzi.
Nenga, kama ambavyo anajulikana kwa jina la kimajazi aliashiria kwamba asilimia kubwa ya wanawake huchepuka katika ndoa zao, iwe ameolewa kwa maskini au tajiri.
Lakini pia aliweza kubainisha tofauti kati ya uchepukaji wa matabaka hayo mawili.
Baba huyo wa mtoto mmoja ambaye pia ni mume wa msanii Nandy alisema kuwa hata kama wanawake karibia wote huchepuka, yule ambaye ameolewa na tajiri anaweza chepuka lakini hawezi kuiacha ndoa yake lakini yule wa maskini anaweza kuchepuka na kuiacha ndoa yake baada ya kupata unafuu wa maisha upande wa pili alikoenda kuchepuka.
“Kitu kimoja ambacho nikuambie, ukiwa na pesa, yaani ukiwa na hela… sababu watu wanasema tajiri anachitiwa na maskini vile vile anachitiwa, hatujui wanawake wanataka nini. Lakini ngoja mimi niwaambie, ukiwa na hela ni rahisi mwanamke anaweza akakuchiti lakini ni ngumu kukuacha lakini ukiwa maskini hauna hela, mwanamke anaweza akakuchiti na kukuacha,” alisema.
Billnass ameyasema haya kukiwa ni miezi kadhaa baada ya kugonga vichwa vya habari alipotambulisha wazi penzi lake na Nandy.
Kwa mujibu wa maoni ya wengi, walikuwa wanahisi kwamba Billnass hamfikii Nandy kiutajiri hadi msanii Baba Levo akatunga wimbo aliomshirikisha Mbosso wakimtambia Billnass kwamba alifuata Kamseleleko kwa Nandy.
Hata hivyo, Billnass alikanusha kwamba alichokifuata kwa Nandy ni utajiri na unafuu wa maisha bali yeye ni mtu aliyejitosheleza kwa upande wa hela na kwa Nandy ni mapenzi tu.
Kweli kwa maneno yake, wawili hao walishiriki mchakato wa kulipa mahari na kiele chake kikawa ni harusi ya kanisani Nandy akiwa mjamzito kwa mwanao Kenaya ambaye wamemtambulisha mitandaoni kwa mara ya kwanza mwezi jana wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa mwaka mmoja.