Msanii wa injili Christine Shusho azungumzia kitendo cha Diamond kubebwa ndani ya jeneza

Shusho anasema kuwa anaunga tasnia yeyote ya ubunifu

Muhtasari

• Msanii maarufu wa nyimbo za injili  anayetokea Kigoma Tanzania Christine Shusho, amechangia maoni yake kuhusu msanii mwenza nyota wa  nyimbo za bongo Diamond Platinumz ya jinsi alivyoingia jukwaani akiwa ndani ya jeneza

• "Naheshimu tasnia nzima ya sanaa Tanzania maana ni wabunifu sana,kwa hivyo chochot wafanyacho ikiwa ni ubunifu naunga mkono."

Photo Cautesy
Photo Cautesy

Msanii maarufu wa nyimbo za injili  anayetokea Kigoma Tanzania Christine Shusho, amechangia maoni yake kuhusu msanii mwenza nyota wa  nyimbo za bongo Diamond Platinumz ya jinsilivyoingia jukwaani akiwa ndani ya jeneza.

Kwenye mahojiano yake ya moja kwa moja na SPM BUZZ Shusho alieleza kuwa anaunga mkono sana swala la ubunifu.

Alieleza kuwa nchi ya Tanzania ni nchi ambayo inashiriki sana kwa ubunifu hasa katika sanaa ya muziki na kusema kuwa anaunga hilo mkono.

Shusho alisema kuwa, ikiwa kuingia jukwaani kwa msanii Diamond  akiwa ndani ya jeneza ni mbinu ya ubunifu basi anaunga hilo mkono kwa;

"Naheshimu tasnia nzima ya sanaa Tanzania maana ni wabunifu sana,kwa hivyo chochot wafanyacho ikiwa ni ubunifu naunga mkono."

Haya yanajiri baada ya siku nne zilizopita ambapo msanii huyo Diamond Platinumz aliingia jukwaani akiwa ndani ya jeneza katika hafla ya bendi ya wasafi.

Mnamo Septemba 11, Mwimbaji huyo wa nyimbo  za Bongo, aliwasisimua mashabiki wake kwa onyesho la kutisha mjini Lindi,wilaya ya Raungwa  ambako alipanda jukuani akiwa amebebwa kwenye jeneza .

Majeneza kadhaa yalibebwa hadi jukwaani na wanaume waliovalia mavazi ya kidini yenye kofia kama vile wanafanya aina fulani ya tambiko la kishetani.

Utendji huu uliwafanya wahafidhuni wengi kumhutumu Platinumz kuwa naabudu shetani.

Hata hivyo jambo hili lilipelekea msanii huyo kukiri kuwa alikuwa amehofia zaidi kuigiza akiwa ndani ya jeneza hilo

"Kutoka kwenye jeneza kulikua tukio la kichaa jana usiku,niliogopa sana!"

Tamasha hilo la wasafi  festivals hushirikisha  wasanii mblimbali waliosainiwa na Wasafi Records pamoja na wanamuziki wengine mashuhuri kutoka Tanzania na muziki wa afrika mashariki