logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ibraah afunguka kupitia maisha magumu katika muziki wake Konde Gang kwa Harmonize

Ibraah aliwataka mashabiki kumpa kumbato la kishua kwa kustream wimbo huo.

image
na Radio Jambo

Makala15 September 2023 - 10:11

Muhtasari


• Ibraah alibainisha kwamba wimbo huo ndio wake wa kwanza kutoa mwaka huu na kuwaomba waendelee kumpa sapoti mashabiki.

• Bosi wake Harmonize pia aliupaisha wimbo huo kwenye Instagram yake yenye wafuasi takribani milioni 10 na kusema kwamba amerudi kwa kishindo.

Ibraah

Baada ya kimya cha Zaidi ya mwaka mmoja, hatimaye msanii Ibraah amewakata kiu mashabiki wake kwa kuachia kibao kimoja kwa jina Hapa.

Ibraah kupitia insta story yake aliandika ujumbe mrefu wenye ukakasi akidokeza kwamba maisha yake ya Sanaa kwa sasa yako katika wakati mgumu Zaidi.

Msanii huyo ambaye hivi majuzi bosi wake – Harmonize – alisema kwamba kimya chake cha muda mrefu kimechangiwa na tofauti za kimaokoto na kampuni ya kusambaza kazi za wasanii, Zikki Media, alidokeza kwamba alibainisha haya ila hakuweza kuzungumzia kwa kina Zaidi kuhusu ugumu huo wa Sanaa yake.

Ibraah aliwataka mashabiki kumpa kumbato la kishua kwa kustream wimbo huo mmoja kwenye majukwaa yote ya kidijitali, akisema kuwa ni wajibu wake kuwapa burudani licha ya kwamba hajakuwa na uwezo wa kufanya hivyo kwa miezi kadhaa sasa.

“Maisha ya Sanaa yangu kwa sasa hivi ni magumu sana ila nawapenda sana mashabiki wangu na najua kwamba mnanipenda sana ndio maana siku zote nitahakikisha ninatumia wajibu wangu kwenu nikisimama kama kijana wenu mlionipa dhamani ya kuwaburudisha kwa kuwapa muziki mzuri,” Ibraah alisema.

Ibraah alibainisha kwamba wimbo huo ndio wake wa kwanza kutoa mwaka huu na kuwaomba waendelee kumpa sapoti mashabiki.

Bosi wake Harmonize pia aliupaisha wimbo huo kwenye Instagram yake yenye wafuasi takribani milioni 10 na kusema kwamba amerudi kwa kishindo.

Hata hivyo, kilichowashangaza watu ni Ibraah kupakia link ya kuwaelekeza mashabiki kwenye muziki wake katika jukwaa la Zikki – jukwaa ambalo Harmonize alilituhumu kwa kukatalia maokoto ya muziki wa Ibraah kwa Zaidi ya miezi 8.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved