Kwa mara nyingine tena msanii Rayvanny ameotesha upya ugomvi wake na aliyekuwa mpenzi wake Paula Kajala.
Rayvanny ambaye alikuwa anatumbuiza katika usiku wa Wasafi Festival eneo la Songea alikuwa jukwaani ambapo aliimba wimbo wa freestyle akitumba mafamba kwa Paula.
Msanii huyo ambaye wamekuwa wakishambuliana na Paula tangu kuachana kimya kimya mwaka jana alidai kwamba binti huyo wa muigizaji Fridah Kajana Masanja urembo wake si wa asii bali ni wa kulazimisha.
Rayvanny alisema kwamba ameshamsahau kwani sasa ana mtoto mwenye rangi ya ngozi inayong’aa ambayo ni asili, akisema kuwa ya Paula ilikuwa ya kulazimisha kwa vipodozi.
“Sikukumbuki wala sikumiss, usijivimbishe wala sikukumbuki. Mpaka sasa hivi niko na mtoto yuko light, ana bright nishamsahau yule wa zamani mpaka caro light,” Rayvanny alisema huku mashabiki wakicharuka kwamba huyo ni Paula moja kwa moja alikuwa anachokoza.
“Katoka kwa msanii kaenda kwa msanii hivi kwa nini wanawake hamsikii,” aliendeleza akimtupia dongo msanii mwenza Marioo ambaye kwa sasa hivi ndiye wanachumbiana na binti huyo.
Rayvanny alizidi kuwafurahisha mashabiki akisema kwamba ikija kutokea Fahyma amemuacha siku moja basi moja kwa moja ataoa Songea na wala si kwingine.
Paula na mpenzi wake mpya Marioo wameziki kutaradadi mitandaoni kwa kipindi kimoja mrembo huyo akidai kwamba Marioo tayari ameridhia kutoa kima cha shilingi milioni 100 za Tanzania kwa ajili ya kumuoa.