Staa wa Bongo Fleva, Harmonize alikumbana na tukio la aibu alipokuwa akitumbuiza katika eneo la Ruangwa, Lindi wakati wa ziara ya Rais Samia Suluhu.
Ajali hiyo ilitokea muda mfupi baada ya Harmonize kutumbuiza wimbo wake maarufu Teacher.
Mwimbaji alikuwa ameanza kucheza, akionyesha dansi zake za kusisimua alipoanguka ghafla.
Haijabainika kama anguko hilo lilikuwa sehemu ya uchezaji wake lakini aliinuka haraka na kuendelea na uchezaji wake.
Rais Samia alionekana akicheka wakati huo pamoja na watazamaji
Hata hivyo Harmonize ametoa shukrani zake kwa rais Samia kwa kuwaunga mkono wasanii. Aidha aliapa kumuunga mkono mkuu wa nchi katika uongozi wake.
"Thank You Thank You my President ππ Ndani Yako Kuna Huruma Na Upendo!!!! Mkubwa Sanaa!!!! Natambua Na Kuthamini Heshima Hiii Uliyonipatia Mimi & Upendo wako Mkubwa Kwa Wasaniii Na Sanaa Kwa Ujumla π Mungu Akutilie Wepesi Uendelee Kuzigusa Sekta Zote Muhimu Zenye Tija Katika Taifa Lako!!! Hili tukufu Tanzania !!!!! NIKUAHIDI TUU Yakwamba Tunasimama Na wewe Tunatamba Na Wewe!!! Full stop β Mazungumzo Majadiliano TUKUTANE (2030),” aliandika msanii huyo.
Hii hapa video ya tukio hilo;