Diamond ajiita mfalme wa ubunifu baada ya kufanikiwa kujenga gereza jukwaani

Mashabiki wake walimhongera kwa ubunifu safi wengine wakimtaka kukoma kutumia vitu vya kutisha kama kuingia jukwaani akiwa ndani ya jeneza.

Muhtasari

• Diamond alionekana  pamoja na watu wengine waliokuwa wanaigiza kama wafungwa lakini yeye chumba chake kilikuwa kimewekwa mabango ya kutahadharisha.

Diamond
Diamond
Image: Insta

Kwa mara nyingine tena tamasha la Wasafi Festival limeshuhudia ubunifu wa kiwango kingine, safari hii kinara wa tamasha Diamond Platnumz akiongoza kwa kuonesha ubunifu uliokwenda skuli.

Msanii huyo baada ya kusimangwa kwa kuingia jukwaani akiwa ndani ya jeneza, alirudi na ubunifu mwingine na kujenga gereza kwenye jukwaa.

Diamond alionekana  pamoja na watu wengine waliokuwa wanaigiza kama wafungwa lakini yeye chumba chake kilikuwa kimewekwa mabango ya kutahadharisha.

Ghafla msanii huyo aliibuka kutoka kitandani na kuanza kutumbuiza kwa vishindo vya mashabiki ambao walikuwa wanamshangilia kwa ubunifu huo ambao haukutarajiwa.

Diamond alishukuru mashabiki kwa kukumbatia ubunifu huo ambao alisema kuwa mwisho wa siku ulilipa kwa kuona tabasamu na mbwembwe kutoka kwa mashabiki.

“Niligeuza Jukwaa la Wasafi Festival kuwa Gereza la Usalama wa Juu Jana Usiku… Kutoka katikati ya Umati wa Watu na Kizimba ilikuwa ni Uzoefu wa Kichaa. Umati wa watu ulinilipa kwa Nguvu ya Kuunguruma iliyolipuka na kupeperusha Uwanja!!” aliandika katika kipande cha video hiyo.

Mashabiki wake walimhongera kwa ubunifu safi wengine wakimtaka kukoma kutumia vitu vya kutisha kama kuingia jukwaani akiwa ndani ya jeneza.

“Sasa huu ndio ubunifu wa kweli, 🔥🔥🔥 wachana na mambo yale ya majeneza kaka...Kweli Simba ni mmoja ulimwenguni,” mtangazaji Billy Miya alimshauri.

“Wasongea wanakwambia SIMBA utatuuuwaaa sio kwa rahaa hizi unazotupa ,” mwingine aliwambia.

Tazama video ya tukio hilo lililoshabikiwa;