logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu kwa nini msanii Nonini amewaomba Wakenya msamaha

“Inaitaji mtu mwenye nguvu kukiri walikosea na niko tayari kwa matusi yoyote hapo kwa maoni

image
na Radio Jambo

Burudani19 September 2023 - 12:00

Muhtasari


  • Aidha alisema yuko tayari kwa upinzani atakaopokea lakini akabainisha kuwa alikuwa na ujasiri wa kukiri kuwa viongozi hao wamefeli Wakenya.

Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Kenya Nonini  aliomba msamaha kwa Wakenya kwa kuunga mkono serikali ya sasa na baadhi ya viongozi wa kisiasa.

Katika ukurasa wake rasmi wa X, mwimbaji huyo wa genge alisema kuwa mambo hayaendi sawa mwaka mmoja tangu utawala wa sasa uchukue husukani.

"Tukiangalia nyuma jinsi nchi yetu inavyoenda mwaka chini ya mstari na serikali hii. Nataka kuwashirikisha WAKENYA kwa sauti kubwa kwa kuunga mkono serikali hii na baadhi ya viongozi unaowafahamu,” aliandika Nonini.

Aidha alisema yuko tayari kwa upinzani atakaopokea lakini akabainisha kuwa alikuwa na ujasiri wa kukiri kuwa viongozi hao wamefeli Wakenya.

“Inaitaji mtu mwenye nguvu kukiri walikosea na niko tayari kwa matusi yoyote hapo kwa maoni lakini angalau niko bold enough Kukubali mambo Kenya sio poa na baadhi ya viongozi wetu wametuangusha Sana. Poleni sana wakenya wenzangu,” mwanamuziki huyo aliongeza.

Hizi hapa baadhi ya hisia za Wakenya;

Mutwiri:Takes an even bigger man to own up to mistakes. They ran a very deceptive campaign, making all the right noises but it's taken just a year to reveal themselves as con artists/wash wash merchants they always were. 'Of importance is life'

David:  It's very true. Things aren't good in this country. It's only a zombified person who can't see we are headed in the wrong direction.

fearless: Apologies accepted bro ...we all make mistake

Terry:The problem started when they elected uhuruto and Tano tena script was worse ,then came hustler nation worsest,now we are paying heavily weather we voted or no

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved