Mmetamani groom mpya tayari? Akothee auliza watu waki'share picha mzungu akimuangalia

"Mbona mnanifanyia hivo jameni, ama mmetamani groom mwingine tayari? Mlisema yule [Mr Omosh] hana nyumba kwa hiyo tuhepe hivi, sio?" Akothee aliwauliza mashabiki wake.

Muhtasari

• Akothee alivutiwa na jinsi mashabiki wake walivyokuwa wakijadili picha ya mzungu huyo asiyejulikana kwa jina.

• Amekuwa akiwajibu kwa ukali mashabiki wanaoshinda wakimuuliza kuhusu uwepo wa Mr Omosh katika miezi ya hivi karibuni.

Akothee.
Akothee.
Image: Facebook

Wiki jana Akothee aliteuliwa kama balozi wa mauzo wa kampuni ya usafiri wa ndege Skyward na alikuwa mmoja wa watu mashuhuri waliokuwa katika uzinduzi wa safari za ndege kutoka uwanja wa Wilson Nairobi moja kwa moja kwenda Migori.

Katika picha moja ambayo iliwaacha Wakenya na mashabiki wa mjasiriamali huyo wakizungumza, Akothee alionekana akishuka kutoka kwa ndege akiwa amevalia nadhifu lakini kando yako kwa mbali aliweza kuonekana raia mmoja wa kigeni – mzungu – akiwa anamtolea macho.

Wengi walianza kuzua utani kwamba huenda hivi karibuni tena Akothee ataonekana na mzungu huyo kama mpenzi wake mpya, ikiwa ni miezi 5 tu baada ya kufungua harusi ya kufana na mume wake mzungu aliyempa jina Mr Omosh.

Akothee alivutiwa na jinsi mashabiki wake walivyokuwa wakijadili picha ya mzungu huyo asiyejulikana kwa jina, kwa jinsi alivyokuwa akimuangalia pasi na ufahamu wa Akothee kwamba alikuwa anaangaliwa kwa nyuma.

Aliwajibu mashabiki wake kwa utani akiwauliza mbona walikuwa wanahisi kwamba mzungu huyo alikuwa anamuangalia kwa jicho la kumtamani kimapenzi, na kuwauliza kama wanataka awaoneshe mpenzi mwinine mzungu.

“Mbona mnamfanyia balozi hivi hakika? Tulieni mtaharibu hii kitu ilikua tu mzuri . Mumetamani groom mpya tayari?I love you my fans , mambo mengi masaa machache, mlisema yule Hana Nyumba 🤣🤣🤣🤣🤣🤣💃💃💃💃💃💃💃💃💃💃💃💃💃💃💃🤣🤣🤣kwa hivyo tuhepe, sio?” Akothee aliuliza kwa utani.

Itakumbukwa kwa miezi ya hivi karibuni, Akothee hajakuwa akionekana hadharani na mpenzi wake Mr Omosh jambo ambalo limewafanya mashabiki wake wengi kuzua maswali wakimtaka kujibu yuko wapi.

Wengine wamekuwa wakimsakama kwa maswali kuhusu maendeleo ya harusi ya pili ambayo aliahidi mashabiki wake ingefanyika nchini Uswizi kwa kina Omosh lakini baadae bahari hizo zikaingia chini ya zulia.

Hata hivyo, Akothee amekuwa akiwajibu kwa shombo na ukali mwingi mashabiki wanaojaribu kumuuliza huku akiwataka kujishughulisha na yanayowahusu.

Majibu hayo ya kebehi yamewafanya baadhi kuhisi kwamba huenda mambo si mazuri katika uhusiano wao na Omosh na hivyo walipomuona mzungu huyo mwingine akimtolea macho ya kimapenzi walihisi huenda ni fursa nyingine ambayo inamfuata mjasiriamali huyo mama wa watoto 5 ambaye hachelewi kudakia fursa kama hizo.