Pesa ni muhimu sana kwenye mahusiano

Hili linatokana na kujifunza kwake kuhusu nafasi ya hela kwenye uhusiano

Muhtasari

•Ronoh alikariri kwamba hali ambayo alipitia ilimpelekea kuweka pesa kwenye msitari wa mbele katika uhusiano wowote.

Deborah Chebet Ronoh/Instagram
Deborah Chebet Ronoh/Instagram

Mshawishi na muunda maudhui kwa mitandao Deborah Chebet almaarufu Ronoh amekiri kwamba pesa ni muhimu sana katika mahusiano.

Ronoh alikariri kwamba hali ambayo alipitia ilimpelekea kuweka pesa kwenye msitari wa mbele katika uhusiano wowote.

Alieleza kuwa anajutia kuchukulia mapenzi kuwa kila kitu kwa uhusiano wowote na hilo likampa funzo la kuhepuka mahusiano ambayo hayana hela akisema kwamba hela huleta utulivu wa kila kitu katika uhusiano.

"Nilijifunza hilo kwa njia ngumu maana nlidhani kuwa mapendi ndio kila kitu lakini hapana, inabidi tuwe na utulivu wa hela  kwanza ndipo kila kitu kifuate."

Ronoh alibainisha kwamba atamkubali na kumupenda mwanaume ambaye anajituma na anaye miliki ya mali ya aina yake.

"Nikipata mwanaume wa kunirahisishia maisha na mwenye mali nyingi ambaye pia ana kipato kikubwa cha hela, basi naingia naye kwenye mahusiano."

Mshawishi huyu aliwahi kuwa mtangazaji kwenye kituo cha redio cha NRG wakishirikiana pamoja na Charlie Karumi .

Hili linaeleza kwa undani ni kwa nini ndo nyingi huwa zinasambaratika na watu huishia kutengana baada ya muda wa mahusiano ya ndoa.

Swala la hela kwenye ndoa linawasukuma vijana  wa kiume kujikaza zaidi kwa kujituma ili wawe katika nafasi mwafaka ya kukimu mahitaji ya wachumba wao,la sivyo huenda wakaambulia patupu mwisho wa kwisha.

Pia swala hili vilevile linawakatisha moyo vijana wengi kujihusisha kwenye mahusiano wakihofia kusalitiwa kimapenzi kwa wenzao wenye nacho hivyo kusihia kusalia bila wachumba licha ya umri kusonga.

Linaitaji sana watu kujikubali na kuishi kwa uwezo wao na kuvumiliana kwenye mahusiano kwa kustahimili kile walicho nacho. Aidha ni vyema vijana wa kiume kufanya kila juhudi maishani kutafuta ela kwa njia mwafaka na safi ili kukimu familia zao .