logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Siwezi kosa kuwa na mpenzi na venye kuna baridi - Carrol Sonie

Sonie hata hivyo aliweka wazi kwamba kwa sasa hana mpango wowote wa kuongeza mtoto mwingine.

image
na Davis Ojiambo

Burudani19 September 2023 - 09:06

Muhtasari


  • • Sonie hata hivyo aliweka wazi kwamba kwa sasa hana mpango wowote wa kuongeza mtoto mwingine.
Carrol Sonie.

Miaka miwili baada ya kuachana na mpenzi wake Mulamwah kwa njia ya kishari, muigizaji Carrol Sonie amefunguka kuhusu maendeleo ya maisha yake ya mapenzi.

Katika mahojiano na Nicolas Kioko pindi tu baada ya kurudi Nairobi kutoka likizo fupi Mombasa, Sonie alisema kwamba ni kweli yeye hawezi kuwa bila mpenzi akitaja ukali wa baridi ya Nairobi kama kitu ambacho asingeweza kukivumilia.

Hata hivyo, hakuweza kumtaja wala kuweka maelezo yoyote kumhusu lakini aliwaacha mashabiki wake na ahadi kwamba hivi karibuni watapata kumfahamu shemeji wao.

“Mimi si kwamba nilirudia Ex wangu, ni mpenzi wangu ambaye alikuwa ameninyamazia kidogo, ni venye nilikosa jina lingine la kumuita. Tuligombana kidogo ananinyamazia akanilima block kwa wiki moja lakini sasa tumerudiana tuko sawa. Hivi karibuni mtamuona tu msijali. Mimi siwezi kosa kuwa na mtu, na venye kuko na baridi siwezi kosa, yupo,” Sonie alisema.

Sonie ambaye alionekana kuwa mwingi wa furaha alisema kuwa hayuko sokoni kabisa na kukiri kwamba mikononi mwa huyo mpenzi mpya, amepata faraja kubwa ambayo hakuwahi pata hata kwa baba mtoto wake – Mulamwah.

“Niko na furaha sana, sikuwa najua mapenzi yanakuwa na hisia hivi, kupendwa raha,” Sonie alisema akisisitiza kwamba mpenzi huyo si mtu maarufu na wala hawezi rudi kuchumbiana na mtu maarufu.

“Siwezi muonesha mpenzi wangu kwenu mitandaoni, zoea kuona mikono na miguu na nikienda sana labda nitawaonesha maskio yake tu. Si kwamba namficha bali huwa nimechagua maisha yangu ya kimapenzi kuwa ya kibinafsi,” Sonie alisema na kuongeza kwamba alijifunza kutokana na penzi lililomwagika la Mulamwah.

Sonie hata hivyo aliweka wazi kwamba kwa sasa hana mpango wowote wa kuongeza mtoto mwingine, akisema mfumko wa bei za bidhaa umekuwa mbaya kiasi kwamba kufikiria kuongeza mtoto mwingine ni wazo gumu ambalo haliwezi kupata upenyo katika kichwa chake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved