Mwana muziki Kelvin Bahati almaarufu Bahati amepata pigo kubwa baada ya wimbo wake kufutwa tukoka jukwaa la YouTube baada ya mtayarishaji wa miziki anayetambulika kama Genius Jinix66 wa Tanzania kudai haki miliki za wimbo huo.
Hi ni baada ya Bahati kuachilia wimbo wake mpya wa 'HUYU' juma lililopita.
Baada ya mtayarishaji huyo kuusikia wimbo huo alikereka zaidi na kusema kwamba msanii Bahati alimwiga katika wimbo huo akidai wimbo huo alikua ameufanya yeye mwenyewe.
Genius alisema kuwa Bahati ameiga wimbo wake unaojulikana kama 'JUU' ambao amemshirikisha msanii Jay Melody.
Kabla wimbo huo haujafutwa Genius alitoa onyo akisema;
"Nikiishusha hii nyimbo nani atanilaumu, kutengeneza sauti si jambo jepesi jamani,tunaumizwa sana akili, hii ni mara ya pili mdundo wangu wanauiga, nikiongea sijui naonekana aje."
Hata hivyo alisema Bahati alifanya hivyo bila idhini yake kwani hakumjulisha.
"Bahati kaka ungeutaka huu mdundo ungeniarifu tu, ningekutengenezea kuliko kufanya hivi, nawapenda sana Kenya kwa sababu ni nyumbani pia ila tusifanyiane hivi tafathali."
Kisha ujumbe uliochapishwa kwenye YouTube ya Bahati ulisoma kama ifuatavyo;
"Video hii haipatikani tena kwa sababu ya dai la hakimilik na Ginius Jinix66."
Msanii Bahati baada ya kuona hatua hizo alijibu kwa mshangao na kusema;
"Shambulizi lingine kutoka Tanzania, Ginius Jix 66 ni nani? alifuta kwa nia mbaya wimbo wangu kwenye YouTube ambao ni nambari mbili kwa kuenea."
Msanii Jay Melody alikuWa ametabiri kwamba kuna uwezekano wimbo huo kuigwa baada ua kutokea.