logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kate Actress arudisha mapenzi katika kunyanyua vyuma baada ya kuachana na mumewe

Wengine walisema ni njia moja ya kujaribu kujisahaulisha kutokana na kuvunjika kwa uhusiano.

image
na Radio Jambo

Makala20 September 2023 - 10:06

Muhtasari


• Jumanne alasiri, Kate Actress aligonga vichwa vya habari baada ya kupakia jumbe kwa mashabiki kwamba yeye na Phil waliachana.

Kate Actress.

Catherine Kamau, maarufu kama Kate Actress amerudisha mapenzi yake katika kunyanyua vyuma kwenye gym, siku moja baada ya kuweka wazi kwamba yeye na mume wake Phillip Karanja walishafikia uamuzi wa kutengana.

Mapema Jumatano asubuhi, Kate alipakia video kwenye Instastoryes zake akiwa kwenye gym akiwa amevalia long’i ya rangi nyeupe na blausi nyeusi.

Kate Actress alionekana kujishaua ili kuwaaminisha mashabiki wake kwamba ameshasahau yaliyopita huku akionekana kuanza kuachia jumbe za kuhimiza nyuma kwa mbaali wimbo wa kutia moyo ukisikika.

“Natumai unajua jinsi ulivyo mjasiri, wa maana, mwenye kung’aa na mwenye uwezo wa ajabu kama ambavyo ulivyo kawaida, hata kama huwa hujihisi hivyo muda wote,” Kate Actress aliandika ujumbe.

Kuonekana kwake gym kulivutia maoni kinzani kutoka mwa watumizi wa mitandao ya kijamii ambao baadhi wanahisi ni kijirudisha kwenye karakana ili kufinyangwa upya tayari kwa kurudi sokoni tena kujaribu mapenzi.

Wengine walisema ni njia moja ya kujaribu kujisahaulisha kutokana na kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye sit u alikuwa mpenzi wake bali pia mshirika wake wa kibiashara.

Jumanne alasiri, Kate Actress aligonga vichwa vya habari baada ya kupakia jumbe kwa mashabiki kwamba yeye na Phil waliachana kitambo lakini kwa muda wote walikuwa wameamua kuliweka suala hilo nyuma ya pazia mbali na mapaparazzi.

Hata hivyo, walisema kwa pamoja kwamba kuvunjika kwa uhusiano wao si mwisho wa urafiki, wakisema kuwa watazidi kushirikiana katika kulea watoto lakini pia kushirikiana katika biashara ya kutoa filamu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved